Synopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodes
-
21 AGOSTI 2025
21/08/2025 Duration: 09minNchini Tanzania Programu ya Pamoja ya Kigoma, (KJP) inayotekelezwa kwenye mkoa huo ulioko magharibi mwa Tanzania kwa lengo la kujengea uwezo wa kuhimili changamoto zitokanazo na uwepo wa wakimbizi unaendelea kujengea uwezo wenyeji na hivi karibuni zaidi ni mradi wa kuongezea thamani zao la alizeti. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi anakupasha zaidi.
-
Ukanda wa Gaza unaongoza duniani kwa watu waliokatika viungo
20/08/2025 Duration: 02minMaelfu ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ambao wamepoteza viungo vyao vya mwili na wanakabiliwa na hali mbaya ya maisha na matatizo makubwa ya kiafya kutokana na ukosefu wa huduma bora za matibabu na viungo bandia wanazohitaji sana. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
-
Ukatili wa kijinsia katika mizozo
20/08/2025 Duration: 03minMsikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa leo tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani kujadili hali hii inayozidi kuongezeka, na kushuhudia jinsi waathirika wanavyobaki bila msaada wa kutosha kutokana na ukosefu wa rasilimali.Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa na Mwakilishi wake imeonesha ongezeko kubwa la kesi za ukatili wa kingono, jambo linaloibua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji na huduma kwa manusura. Leah Mushi ametuandalia makala ifuatayo ikieleza hayo kwa kina.
-
20 AGOSTI 2025
20/08/2025 Duration: 09minJaridani leo tunaangazia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, na hali ya kibinadamu Gaza na majeraha kwa wenyeji. Makala tunaangazia ukatili wa kingono na mashinani tunakwenda Sudan kumulika jinsi wanavyokabiliwa na unyanyasaji huo wa kingono.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema Afrika inahitaji mageuzi makubwa ya Baraza la Usalama na mfumo wa kimataifa wa fedha ili kufanikisha maendeleo yake na nafasi yake duniani. Akihutubia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, Guterres ameweka vipaumbele vitano.Maelfu ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ambao wamepoteza viungo vyao vya mwili na wanakabiliwa na hali mbaya ya maisha na matatizo makubwa ya kiafya kutokana na ukosefu wa huduma bora za matibabu na viungo bandia wanazohitaji sana.Tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani ku
-
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aweka vipaumbele vitano kwa maendeleo ya Afrika
20/08/2025 Duration: 01minKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema Afrika inahitaji mageuzi makubwa ya Baraza la Usalama na mfumo wa kimataifa wa fedha ili kufanikisha maendeleo yake na nafasi yake duniani. Akihutubia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, Guterres ameweka vipaumbele vitano. Flora Nducha anafafanua zaidi
-
19 AGOSTI 2025
19/08/2025 Duration: 10minJaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika umuhimu wa wahisani. Pia tunaangazia siku ya Wahudumu wa Kibinadamu Duniani tukikuletea ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaomulika haki zao, na hali ya usalama nchini DRC.Leo ni Siku ya Wahudumu wa Kibinadamu Duniani na Umoja wa Mataifa unasema mwaka 2024 ulikuwa mbaya zaidi, baada ya wahudumu 383 kuuawa kote duniani, hasa Gaza na Sudan. Mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, amesema “Hata shambulio moja dhidi ya mhudumu wa misaada ni shambulio dhidi yeto sote.” Naye Katibu Mkuu António Guterres ameongeza kuwa “Shambulio dhidi ya wahudumu wa misaada ni shambulio dhidi ya ubinadamu hebu tuchukue hatua kwa ajili ya ubinadamu.Huko Geneva Katika hafla maalum ya kuadhimisha siku hii, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Volker Türk, amewakumbuka waliopoteza maisha, wakiwemo wahudumu 22 waliouawa Baghdad mwaka 2003, na kuongeza “Kamwe hatutaacha kusisitiza kwamba serikali au nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wafanye kazi
-
Gaza ni tishio lililo kimya - Dkt. Younis
18/08/2025 Duration: 03minUmoja wa Mataifa umetenga siku maalum ya kuwashukuru watoa huduma za misaada ya kibinadamu na siku hiyo ni Agosti 19 kila mwaka. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu zinaeleza kuwa mwaka huu wa 2025, watu milioni 305.1 kutoka nchi 72 wanahitaji usaidizi wa kibinadamu ambao utagharibu dola bilioni 47.4. Takwimu hizi zinaonesha umuhimu na uhitaji wa watoa huduma wa kibinadamu.Kuelekeza maadhimisho hayo hapo kesho Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masual ya Watoto UNICEF limetengeneza makala inayoangazia watoa huduma wa misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kimabavu na Israel. Leah Mushi anatujuza kilichopo katika makala hiyo.
-
Mradi wa IFAD na ILO wadhihirisha nguvu ya vijana kwenye kilimo vijijini
18/08/2025 Duration: 01minMashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la ajira, ILO na mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD yanatekeleza mradi wa ProAgro YOUTH unaolenga kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini.
-
18 AGOSTI 2025
18/08/2025 Duration: 09minJaridani leo tunaangazia amani na usalama nchini Ukraine, na ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini. Makala tunaangaazia wahudumu wa kibinadamu Gaza, na mashinani tunamulika afya kwa wanawake wajawazito nchini Tanzani.Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine yaliyofanyika usiku kucha, ikiwemo katika miji ya Kharkiv na Zaporizhzhia, yameripotiwa kuua watu 10 wakiwemo watoto watatu, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo.Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la ajira, ILO na mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD yanatekeleza mradi wa ProAgro YOUTH unaolenga kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini.Makala Umoja wa Mataifa umetenga siku maalum ya kuwashukuru watoa huduma za misaada ya kibinadamu na siku hiyo ni Agosti 19 kila mwaka. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu zinaeleza kuwa mwaka huu wa 2025, watu milioni 305.1 kutoka nchi 72
-
Vijana wengi zaidi wapoteza maisha na kujeruhiwa katika mashambulizi ya Urusi huko Ukraine: UNICEF
18/08/2025 Duration: 01minMashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine yaliyofanyika usiku kucha, ikiwemo katika miji ya Kharkiv na Zaporizhzhia, yameripotiwa kuua watu 10 wakiwemo watoto watatu, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo. Flora Nducha na taarifa zaidi
-
Kutoka kufanya kazi za ndani hadi kumiliki kampuni ya usafi wa mazingira
15/08/2025 Duration: 04minKutana na Godlove Makunge, kijana huyu wa kitanzania ambaye safari ya maisha yake imedhihirisha kuwa chochote unachoweka nia na utashi kitafanikiwa. Godlove ambaye elimu yake ni ya kidato cha nne, hakuweza kuendelea na masomo zaidi. Alichukuliwa na mtu mmoja afanye kazi za ndani kutoka Morogoro hadi Lindi na kisha akaishia Mtwara, kusini-mashariki mwa Tanzania ambako huko aliona fursa ya kujipatia kipato kutokana na taka zilizokuwa zinasambaa mitaani. Aliasisi kampuni ya usafi na mazingira iitwayo Shikamana Investment. Sasa kampuni yao ya ubia imeajiri vijana 6. Alishiriki mafunzo ya uchumi rejeleshi yaliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP mkoani Mtwara. Sawiche Wamunza, Sawiche Wamunza Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimkakati UNDP alizungumza na Bwana Makunge baada ya mafunzo hayo ili afahamu amejifunza nini.
-
Mazungumzo kuhusu mustakabali wa plastiki yaahirishwa bila muafaka
15/08/2025 Duration: 01minSiku 10 za mkutano wa Kamati ya Kimataifa ya Majadiliano (INC) ya kuandaa Mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, ikiwemo katika mazingira ya bahari, zimemalizika huko Geneva, USwisi bila muafaka kwenye nyaraka tarajiwa, ambapo mkutano umeahirishwa hadi tarehe itakayotangazwa baadaye. Sabrina Said ana taarifa zaidi.
-
15 AGOSTI 2025
15/08/2025 Duration: 09minJaridani leo tunaangazia mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, na vidokezo vya malezi salama ya watoto. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Chad, kulikoni?Siku 10 za mkutano wa Kamati ya Kimataifa ya Majadiliano (INC) ya kuandaa Mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, ikiwemo katika mazingira ya bahari, zimemalizika huko Geneva, Uswisi bila muafaka kwenye nyaraka tarajiwa, ambapo mkutano umeahirishwa hadi tarehe itakayotangazwa baadaye.Kuwa mzazi si rahisi kila wakati, lakini usaidizi unaofaa unaweza kuleta mabadiliko ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limekuwa likiendesha mafunzo kwa wazazi juu ya namna bora za kulea watoto. Alinune Nsemwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kutoka UNICEF nchini Tanzania ameeleza vidokezo vitatu muhimu vya kuwalea watoto ambavyo vinaweza kuleta utofauti mkubwa.Makala ninakukutanisha na Sawiche Wamunza
-
UNICEF: Vidokezo muhimu vya malezi bora kwa watoto
15/08/2025 Duration: 01minKuwa mzazi si rahisi kila wakati, lakini usaidizi unaofaa unaweza kuleta mabadiliko ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limekuwa likiendesha mafunzo kwa wazazi juu ya namna bora za kulea watoto. Alinune Nsemwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kutoka UNICEF nchini Tanzania ameeleza vidokezo vitatu muhimu vya kuwalea watoto ambavyo vinaweza kuleta utofauti mkubwa.
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno “MAHAZAMU”
14/08/2025 Duration: 01minKatika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana ya neno “MAHAZAMU”.
-
-
Vijana waeleza mustakabali wa maisha yao na iwapo wangependa kuwa wazazi
13/08/2025 Duration: 02minWakati dunia ikiendelea kugubikwa na changamoto mbalimbali ikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi na hali mbaya za kiuchumi, vijana wamepaza sauti kueleza wasiwasi wao wa kuwa na Watoto siku za usoni. Tuungane na Leah Mushi katika Makala hii aliyotuandalia kutoka kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA ambayo iliwahoji vijana kutaka kufahamu iwapo wangependa kuwa na Watoto kwa siku za usoni.
-
Mahakama ya kuhamahama yaleta haki na amani Greater Pibor nchini Sudan Kusini
13/08/2025 Duration: 01minMahakama ya kuhamahama iliyopelekwa katika eneo la utawala la Greater Pibor, Kaunti ya Pibor jimboni Jonglei Mashariki mwa Sudan Kusini imeleta haki na amani kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo. Anold Kayanda anatupasha kwa kina
-
13 AGOSTI 2025
13/08/2025 Duration: 09minJaridani hii leo tunaangazia hakiza binadamu nchini Uganda, na mahakama ya kuhamama kwa ajili ya amani Sudan Kusini. Makala tunaangazia vijana na mpango wa wa kuwa wazazi siku zijazo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya kumulika vijana wakulima.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kunyimwa dhamana mara kwa mara katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Mahakama ya kuhamahama iliyopelekwa katika eneo la utawala la Greater Pibor, Kaunti ya Pibor jimboni Jonglei Mashariki mwa Sudan Kusini imeleta haki na amani kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo.Makala wakati hapo jana dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA liliwahoji vijana iwapo wangependa kuwa na watoto hapo baadaye.Na katika mashinani fursa ni yake Emily, mwanachama wa kikundi cha vijana wakulima nch
-
Tunatiwa hofu kubwa na kitendo cha Besigye kuendelea kunyimwa dhamana Uganda
13/08/2025 Duration: 02minOfisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kunyimwa dhamana mara kwa mara katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.