Habari Za Un

26 SEPTEMBA 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo ni hotuba ya Israeli kwenye mjadala mkuu wa baraza kuu, nini kilitokea? Kijana daktari mwanaharakati kutoka Ghana aishiye Uingereza akiwa UNGA80 na matumaini mapya ya kinga dhidi ya maambukizi ya VVU.Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia katika siku yake ya nne hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo Ijumaa, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa wa kwanza kuzungumza akitumia muda wake mwingi kushambulia wanamgambowa kipalestina, Hamas na kutetea kila uamuzi wa Israel. Anold Kayanda ameifuatilia hotuba hiyo kwa kina. Karibu Anold utupe japo kwa muhtasari.Tukisalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, moja ya mikutano ya ngazi ya juu iliyofanyika kando ya mjadala mkuu wa Baraza Kuu, ni ule wa kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa program ya Umoja wa Mataifa kuhusu vijana, mkutano ukileta vijana kutoka kona mbali mbali za dunia. Miongoni mwao ni daktari wa tiba na mwanaharakati wa kijamii wa vijana kutoka Uingerez