Synopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodes
-
Jifunze Kiswahili: Maana za maneno "USHINZI NA USHENZI"
02/10/2025 Duration: 47sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana za maneno "USHINZI NA USHENZI"
-
02 OKTOBA 2025
02/10/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ujumbe wa Omon Ukpoma-Olaiya, Kiongozi wa Uwekezaji wa UNCDF kwa Kanda ya Afrika Mashariki, Kusini na Nchi za Kiarabu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi neno la wiki.Haiti, hali ya kibinadamu imefika kiwango cha hatari, amesema Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk. Akihutubia Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Türk amesema Haiti imefika kiwango cha kulipuka kutokana na ukatili na ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu. Amesisitiza kuwa “Tunaweza na lazima kubadili hali hii kwa ajili ya watu wa Haiti,” akiongeza kuwa “bila hatua za haraka hali mbaya zaidi huenda ikaja kwa Haiti na eneo zima.”Tukielekea Mashariki ya Kati huko Gaza, janga la kibinadamiu linaongezeka ambapo mashambulizi yanayoendelea yameathiri vibaya upatikanaji wa chakula na maji. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA, limeripoti kuwa usambazaji wa chakula kilichopikwa kaskazini mwa Gaza umepungua kwa asilim
-
Gaza - Matumizi ya plastiki kama nishati ya kupikia yasababisha kuenea kwa magonjwa ya kupumua
01/10/2025 Duration: 02minHuko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanawake katika eneo la Deir al- Balah wanalazimika kutumia majiko ambayo wanachochea taka za plastiki na makaratasi ili kupota moto wa kuweza kupikia chakula. Hali hiyo imesababisha kuenea kwa magonjwa ya kupumua kama vile numonia na pumu. Tuungane na Leah anayetujuza zaidi
-
Lazima tutambue mchango wa wazee katika kuunda jamii zenye haki - UN
01/10/2025 Duration: 03minTuanzie hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako kumefanyika tukio maalum la kuadhimisha siku ya wazee duniani leo Oktoba Mosi, kaulimbiu ikiwa Wazee Wanaendesha Hatua za Kijamii na Kimaisha: Matamanio Yetu, Ustawi Wetu na Haki Zetu. Anayekupeleka ukumbini ni Flora Nducha.
-
01 OKTOBA 2025
01/10/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Wazee duniani na mchango wao kwa jamii, hali ya afya katika ukanda wa Gaza, na simulizi ya Balozi Mwema wa UNICEF, Angelique Kidjo.Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako kumefanyika tukio maalum la kuadhimisha siku ya wazee duniani leo Oktoba Mosi, kaulimbiu ikiwa Wazee Wanaendesha Hatua za Kijamii na Kimaisha: Matamanio Yetu, Ustawi Wetu na Haki Zetu. Anayekupeleka ukumbini ni Flora Nducha.Huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanawake katika eneo la Deir al- Balah wanalazimika kutumia majiko ambayo wanachochea taka za plastiki na makaratasi ili kupota moto wa kuweza kupikia chakula. Hali hiyo imesababisha kuenea kwa magonjwa ya kupumua kama vile numonia na pumu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linatoa wito kwa viongozi wa Afrika kufanya uwekezaji wa kifedha wa busara utakaowezesha watoto kupata ujuzi wa msingi wa kujifunza na mustakabali wenye nguvu kwa bara la Afrika. Balozi Mwema wa UNICEF, Angeli
-
Angelique Kidjo, Mwanamuziki, asimulia safari yake ya elimu akiunga mkono wito wa UNICEF kwa viongozi wa Afrika
01/10/2025 Duration: 03minShirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linatoa wito kwa viongozi wa Afrika kufanya uwekezaji wa kifedha wa busara utakaowezesha watoto kupata ujuzi wa msingi wa kujifunza na mustakabali wenye nguvu kwa bara la Afrika. Balozi Mwema wa UNICEF, Angelique Kidjo, katika kuunga mkono wito huo anasimulia safari yake kutoka kujifunza alfabeti hadi kuimba kwa ulimwengu mzima. Anold Kayanda anaeleza zaidi.
-
EAC yasisitiza usalama, uchumi na masuala ya kidijitali katika Mjadala Mkuu wa UNGA80
30/09/2025 Duration: 09minKama unavyofahamu Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 umekunja jamvi rasmi jana Jumatatu. Na tumepata fursa ya kuzungumza na washiriki mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Veronica Nduva ambaye alizungumza na Flora Nducha kandoni mwa mjadala huo kuangazia mchango wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kutekeleza ajenda ya Umoja wa Mataifa ikiwemo masuala ya Amani na usalama, maendeleo na ushirikiano wa kikanda. Ungana nao.
-
30 SEPTEMBA 2025
30/09/2025 Duration: 12minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ujumbe wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Veronica Nduva ambaye alizungumza na Flora Nducha kandoni mwa UNGA80. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Ikiwa ni zaidi ya miaka minane tangu zaidi ya wakimbizi 750,000 waislamu wa kabila la warohingya wakimbie Myanmar kuelekea kwenye kambi kubwa nchini Bangladesh, mgogoro huo bado haujapatiwa suluhisho na leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa viongozi wamekutana kusaka suluhu ya kudumu kwa warohingya na makabila mengine madogo nchini Myanmar. Katibu Mkuu Antonio Guterres kupitia Afisa Mtawala Mkuu wa UN Courtenay Rattray amesema, “mgogoro huu, ambao umezidi kuongezeka tangu mapinduzi ya kijeshi Myanmar ya mwaka 2021, unasigina haki za binadamu, utu na usalama wa mamilioni ya watu na unatishia uthabiti wa kikanda. Haitoshi tu kutathmini hali ilivyo. Tunapaswa pia kuendeleza mshikamano na kubuni suluhisho.”Amani nchini DRC imesalia bado ahadi, ni kauli ya Bintou Keita, Mwakil
-
Mizozo inayoendelea duniani, uchumi Afrika vyatawala siku ya mwisho ya mjadala mkuu
29/09/2025 Duration: 03minViongozi wa mataifa ya nchi wanachama 16 waliopanda kwenye mimbari ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Jumatatu ya tarehe 29 Septemba 2025 ambayo ndio ukomo wa Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, (UNGA80) wamepaza sauti zao kuhusu masuala mbalimbali yanayokumba dunia hivi sasa ikiwemo vita Gaza, na hali ya kiuchumi Afrika.
-
Ili Afrika ‘iimarike kiafya’ inabidi isiwe tegemezi kwenye masuala ya kifedha: Dkt. Ntuli Kapologwe
29/09/2025 Duration: 03minHapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA80, inafanyika mikutano mingine ya pembezoni kujadili masuala mengine ya kusongesha maendeleo ya ulimwengu. Wiki iliyopita tulizungumza na Dkt. Ntuli Kapologwe Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA wakati alipokuwa akisubiri kushiriki mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kujadili jinsi ya kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya. Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza tena na Dkt. Kapologwe mara tu baada ya mkutano huo
-
29 SEPTEMBA 2025
29/09/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunaangazia leo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 tukimulika hotuba za viongozi na mikutano mingine ya pepmbezoni kuhusu malengo ya maendeleo enedelevu, SDGs.Viongozi wa mataifa ya nchi wanachama 16 waliopanda kwenye mimbari ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Jumatatu ya tarehe 29 Septemba 2025 ambayo ndio ukomo wa Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, (UNGA80) wamepaza sauti zao kuhusu masuala mbalimbali yanayokumba dunia hivi sasa ikiwemo vita Gaza, na hali ya kiuchumi Afrika.Leo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 hotuba za viongozi ukifunga pazia, Afrika imeweka bayana kauli moja ya mshikamano, kwamba lazima iwe na viti na sauti kwenye Baraza la Usalama na kuahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha dhamira hiyo inatimia. Mchakato ulishaanza na unaendelea kuelekea lengo hilo kama ambavyo Balozi Ekitela Lokaale mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa alivy
-
Afrika imedhamiria kuhakikisha ina sauti na nafasi Baraza la Usalama la UN: Balozi Lokaale
29/09/2025 Duration: 03minLeo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 hotuba za viongozi ukifunga pazia, Afrika imeweka bayana kauli moja ya mshikamano, kwamba lazima iwe na viti na sauti kwenye Baraza la Usalama na kuahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha dhamira hiyo inatimia. Mchakato ulishaanza na unaendelea kuelekea lengo hilo kama ambavyo Balozi Ekitela Lokaale mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa alivyomfahamisha
-
UNGA80 na maelezo kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs - Dkt. Mohamed Yakub Janabi
26/09/2025 Duration: 07minMada hii kwa kina inamulika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs unaoendelea kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80. Flora Nducha wa Idhaa hii amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wazungumzaji wa Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Mohamed Yakub Janabi
-
VVU: Sindano ya kuzuia kupatikana kwa bei nafuu kuanzia mwaka 2027
26/09/2025 Duration: 02minMakubaliano yaliyosimamiwa na mashirika ya kimataifa, likiwemo UNITAID ambalo ni shirika tanzu la shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, halikadhalika Mpango wa afya wa Clinton (CHAI), Wits RHI na Maabara ya Dkt. Reddy, yanalenga kuhakikisha upatikanaji wa Lenacapavir kwa gharama nafuu.Dawa hii, inayodungwa mara mbili pekee kwa mwaka, imeonesha ufanisi mkubwa katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU, jambo muhimu hasa kwa wale wanaopata changamoto kutumia dawa za kila siku.Video ya UNITAID inaonesha maabara yenye teknolojia ya hali ya juu, ambamo wanasayansi wanaandaa dawa hiyo inayotarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kwa mamilioni ya watu walio katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNITAID, Tenu Avafia, anasema hatua hii ni ushindi mkubwa kwa jamii zinazohitaji kinga ya muda mrefu dhidi ya VVU."Tumeitikia wito kutoka kwa jamii na nchi tunazohudumia kwa kuhakikisha dawa hii inapatikana kwa gharama nafuu. Tunatarajia usambazaji wa toleo la bei nafuu la daw
-
Mwanaharakati Dkt.Owusu: Ni wakati wa sauti zetu vijana zisikilizwe kwa vitendo
26/09/2025 Duration: 02minKatika Mkutano wa Vijana wa Umoja wa Mataifa unaofanyika kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 unaoendelea hapa New York, viongozi vijana kutoka duniani kote wanataka uwakilishi mkubwa katika maamuzi ya kimataifa.Miongoni mwao ni daktari wa tiba na mwanaharakati wa kijamii wa vijana wa Uingereza na Ghana, Dkt. Khadija Owusu ambaye amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili.Owusu, ambaye pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Akaya inayowakilisha wasichana wa zama hizi, anasema vijana hawapaswi kuzungumziwa tu, bali wajumuishwe moja kwa moja katika kuandaa Suluhu za changamoto zinazoihusu dunia wakiwemo na wao "Mara nyingi tunazungumza kuwa tunataka ushiriki zaidi wa vijana wakati umefika wa kuacha kuzungumza tu kuhusu kuhitaji vijana wengi, bali tuwe na vijana wengi."Niko hapa kuwakilisha maelfu ya wasichanaAnasema ushiriki wake katika mkutano huu wa ngazi ya juu wa vijana si wa kibinafsi tu, bali unaakisi sauti za wasichana na vijana wengi wanaosaidiwa
-
UNGA80:Hotuba ya Netanyahu yakumbana na upinzani, yeye augeuza ukumbi kuwa darasa
26/09/2025 Duration: 03minMjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia katika siku yake ya nne hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo Ijumaa, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa wa kwanza kuzungumza akitumia muda wake mwingi kushambulia wanamgambowa kipalestina, Hamas na kutetea kila uamuzi wa Israel. Anold Kayanda ameifuatilia hotuba hiyo kwa kina. Ilikuwa majira ya saa tatu na dakika chache hivi asubuhi ya leo saa za New York nchini Marekani ambapo Waziri Mkuu wa Isreal Benjamin Netanyahu amepewa fursa ya kuhutubia na ndipo ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukakosa utulivu. Wajumbe kwa makundi walinyanyuka katika viti vyao na kuondoka huku wakiwaacha maafisa wa Israel wakimpigia makofi kiongozi wao na pia nchi zinazoiunga mkono Israel zikasalia katika viti vyao ikiwemo Marekani.Baadhi ya wajumbe watoka njeKatika eneo la walipotakiwa kukaa wawakilishi wa Palestina kulikuwa wazi, huku katika eneo la Iran ikibakia picha iliyokusanya sura
-
26 SEPTEMBA 2025
26/09/2025 Duration: 09minHii leo ni hotuba ya Israeli kwenye mjadala mkuu wa baraza kuu, nini kilitokea? Kijana daktari mwanaharakati kutoka Ghana aishiye Uingereza akiwa UNGA80 na matumaini mapya ya kinga dhidi ya maambukizi ya VVU.Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia katika siku yake ya nne hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo Ijumaa, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa wa kwanza kuzungumza akitumia muda wake mwingi kushambulia wanamgambowa kipalestina, Hamas na kutetea kila uamuzi wa Israel. Anold Kayanda ameifuatilia hotuba hiyo kwa kina. Karibu Anold utupe japo kwa muhtasari.Tukisalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, moja ya mikutano ya ngazi ya juu iliyofanyika kando ya mjadala mkuu wa Baraza Kuu, ni ule wa kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa program ya Umoja wa Mataifa kuhusu vijana, mkutano ukileta vijana kutoka kona mbali mbali za dunia. Miongoni mwao ni daktari wa tiba na mwanaharakati wa kijamii wa vijana kutoka Uingerez
-
25 SEPTEMBA 2025
25/09/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalum inayomulika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs unaoendelea kandoni mwa UNGA80, na tumezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Mohamed Yakub Janabi.Wakati viongozi wa nchi na serikali wanahutubia wakiwa ndani ya jengo la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas ujumbe wake kwa UNGA80 ameutoa kwa njia ya video iliyorekodiwa kutokana na kutopata kibali cha kuingia Marekani. Katika hotuba hiyo amesisitiza kuwa, Ukanda wa Gaza utaendelea kuwa sehemu ya Taifa la Palestina na tuko tayari kuwajibika kikamilifu kwenye uongozi na usalama wa eneo hilo. Hamas hawatokuwa na jukumu lolote kwennye utawala.”.Mapema kabla ya Palestina, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, alihutubia wajumbe akitaka nchi wanachama kujitolea upya kwa misingi ya usawa, mshikamano na ushirikiano wa kimataifa. Amesema hilo ni muhimu kwa kuwa “wakati ambapo hapo awal
-
Taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu - Volodymyr Zelenskyy
24/09/2025 Duration: 03minRais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu wanachoweza kufanya ni kutoa matamko makali pekee na kwamba kwa sasa duniani sheria pekee za Kimataifa haziwezi kusaidia nchi kujilinda bila ya kuwa na silaha pamoja na marafiki wenye nguvu wa kukusaidia. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.
-
ECSA: Diplomasia ya kisayansi kutumika kusongesha Mkataba wa Zama Zijazo Afrika
24/09/2025 Duration: 07minKatika siku ya pili ya Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, kando ya hotuba, viongozi wa nchi 9 wanachama wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA watakuwa na mkutano wa kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya, baada ya kujifunza kutokana na COVID-19 au UVIKO19. Mkurugenzi Mkuu wa ECSA Dkt. Ntuli Kapologwe akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ametaja wanachotarajia kwenye mkutano huo..