Synopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodes
-
UN: Sasa ni wakati wa kutimiza ahadi ya usawa wa kijinsia
07/03/2025 Duration: 03minKatika kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake ambayo huadhimishwa kila mwaka Machi 8 leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika hafla maalum ya kuadhimisha siku hiyo ambayo mwaka huu imebeba maudhui “Kwa wanawake na wasichana wote: haki, usawa, uwezeshaji.” Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women Sima Bahous amesema ni wakati wa kutekeleza kwa vitendo ndoto ya azimio la Beijing miaka 30 iliyopita la kufanya usawa wa kijinsi kuwa hali halisiKwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pamoja na kupongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kusongesha usawa wa kijinsia duniani amesemaNatts….“Hata hivyo, mafanikio haya yaliyopatikana kwa jitihada kubwa bado ni dhaifu na hayatoshi kabisa.Mateso ya muda mrefu, ukatili, ubaguzi na ukosefu wa usawa wa kiuchumi bado vinaathiri jamii zetu.Kila baada ya dakika kumi, mwanamke huuawa na mwenzi wake au mwanafamilia.”Ameongeza kuwa wanawake na wasichana milioni 612 wanai
-
07 MACHI 2025
07/03/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunaangazia maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake, na hali ya wanawake wajawaito nchini Ukraine. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni?Kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8, tathmini mpya ya Umoja wa Mataifa iliyowekwa wazi leo ikiangazia haki za wanawake miaka 30 baada ya Azimio la Beijing inaonesha uwepo wa maendeleo katika usawa wa kijinsia, kama vile sheria dhidi ya ubaguzi na sera jumuishi za kijinsia. Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza uwepo bado wa ubaguzi wa kijinsia uliojikita katika jamii, ukiendelea kuwazuia wanawake na wasichana kupata fursa.Zikiwa zimesalia siku mbili ya leo na kesho kufika tarehe 8 Machi Siku ya Kimataifa ya Wanawake, tunaendelea kuangazia hali ya wanawake duniani. Sharon Jebiichi anatupeleka Ukraine kutukutanisha na Mwakilishi wa muda wa Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu UNFPA nchini humo ambaye anaangazia madhila wanayokutana nayo wanawake wajawazito wa Ukraine.Katika makala Assumpta M
-
Ukraine: Mwakilishi wa UNFPA Ukraine Uller Muller na hali ya wanawake wajawazito nchini humo
07/03/2025 Duration: 01minZikiwa zimesalia siku mbili ya leo na kesho kufika tarehe 8 Machi Siku ya Kimataifa ya Wanawake, tunaendelea kuangazia hali ya wanawake duniani. Sharon Jebiichi anatupeleka Ukraine kutukutanisha na Mwakilishi wa muda wa Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu UNFPA nchini humo ambaye anaangazia madhila wanayokutana nayo wanawake wajawazito wa Ukraine.Ni Ulla Muller, Mwakilishi wa muda wa Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu UNFPA nchini Ukraine, akieleza kuhusu changamoto zinazowakumba wanawake wajawazito wa Ukraine.Anasema, “ninaweza kukuambia hadithi nyingi ambazo zimebaki nami kwa sababu nakutana na wanawake hawa kila mara, na mapenzi yangu kwao hayana mipaka.”Uller Muller anasimulia kisa cha mwanamke mmoja akisema,"Kuna mwanamke anayeitwa Ira ana umri wa miaka 31, na tayari anamlea mtoto mvulana wa umri wa miaka sita. Hivi karibuni aligundua kuwa ni mjamzito tena na anatarajia mapacha watatu. Ni hali ya kutisha na kuchanganya."Bi. Muller anaendelea kueleza kuwa mwanamke huyo aliku
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya methali "Mchawi akifichua mirimo ya wachawi huuawa"
06/03/2025 Duration: 01minLeo katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “MCHAWI AKIFICHUA MIRIMO YA WACHAWI HU UAWA”.
-
06 MACHI 2025
06/03/2025 Duration: 10minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Umoja wa Mataifa kupitia miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP nchini Tanzania, unaolenga kuhakikisha wanawake na wasichana wanajumuishwa kwenye mipango ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kwa kuwajengea uwezo.Kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8, tathmini mpya ya Umoja wa Mataifa iliyowekwa wazi leo ikiangazia haki za wanawake miaka 30 baada ya Azimio la Beijing inaonesha uwepo wa maendeleo katika usawa wa kijinsia, kama vile sheria dhidi ya ubaguzi na sera jumuishi za kijinsia. Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza uwepo bado wa ubaguzi wa kijinsia uliojikita katika jamii, ukiendelea kuwazuia wanawake na wasichana kupata fursa.Ripoti nyingine ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo ikiangazia Sudan imefichua vitendo vya watu kukamatwa kiholela, mateso, na unyanyasaji huko Khartoum vinavyotekelezwa na Vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) na pia Jeshi la Serikali ya Sudan (SAF). Ripoti hiyo imearifu pia kuwa m
-
Hali ya usalama ikidorora DRC, hofu sasa ni mustakabali wa watetezi wa haki za binadamu
05/03/2025 Duration: 01minHali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor leo ametoa wito wa msaada wa dharura na wa vitendo kwa watetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo. Anold Kayanda na taarifa zaidi. (Taarifa ya Anold Kayanda)Mary Lawlor akizungumza leo jijini Geneva-Uswisi amesema, "watetezi wa haki za binadamu mashariki mwa DRC wako hatarini sana kulengwa na kulipiziwa kisasi kwa kazi yao ya kutetea haki za binadamu. Wanahitaji msaada sasa, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa kuhamishwa kwa muda pamoja na familia zao.”Kundi la waasi la M23, limeendelea kusonga mbele katika eneo hilo la mashariki mwa DRC tangu lilipoanza mashambulizi yake mapema mwaka huu, na wale waliorekodi na kufichua ukiukwaji wa haki zao wamekuwa wakilengwa moja kwa moja, amesisitiza Bi. Lawlor."Katika wiki za hivi karibuni nimepokea taarifa nyingi za tahadhari zinazohitaji msaada na nimezungumza moja kwa moja
-
Miaka 30 baada ya Azimio la Beijing kuhusu haki za wanawake, safari bado ni ndefu
05/03/2025 Duration: 02minKuelekea siku ya wanawake duniani itakayoadhimishwa mwishoni mwa wiki hii ambayo ni tarehe 8 mwezi Machi, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women, Sima Bahous, amesisitiza kwamba ahadi zilizowekwa kwenye Azimio la Beijing miaka 30 iliyopita kuhusu haki za wanawake hazipaswi tu kukumbukwa bali zinahitaji kutekelezwa kikamilifu. Flora Nducha anafafanua zaidiAkizungumza wiki hii mjini Geneva Uswisi katika majadiliano ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ya kuadhimisha miaka 30 ya Azimio la Beijing (#Beijing30), Bi. Bahous amebainisha umuhimu wa kuharakisha maendeleo ya usawa wa kijinsia akiwataka viongozi wa dunia kuchukua hatua thabiti ili kuhakikisha haki za wanawake zinapewa kipaumbele wakati wa changamoto zinazoendelea duniani.Amesema “Miaka 30 iliyopita dunia iliweka ahadi ya kusongesha fursa na utu wa wanawake na wasichana wote. Ahadi hiyo haikuwa maneno matupu kwenye karatasi, ilikuwa ramani ya njia na wito wa mshikamano . Na kwa
-
05 MACHI 2025
05/03/2025 Duration: 09minHii leo jarida linamulika wasiwasi kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu nchini DRC, wakati huu hali ya usalama si shwari mashariki mwa nchi; kuelekea siku ya wanawake duniani, Mkuu wa UN Women arejelea Azimio la Beijing; vilabu vya Dimitra nchini DRC vinavyosaidia wanawake na wanaume kuketi pamoja na kutatua changamoto zinazowakabilia; mashinani ni Ramadhani huko Gaza.Hali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor leo ametoa wito wa msaada wa dharura na wa vitendo kwa watetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Kuelekea siku ya wanawake duniani itakayoadhimishwa mwishoni mwa wiki hii ambayo ni tarehe 8 mwezi Machi, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women, Sima Bahous, amesisitiza kwamba ahadi zilizowekwa kwenye Azimio la Beijing miaka 30 iliyopita kuhusu haki za wanawak
-
Vilabu vya Dimitra vyaimarisha usawa wa kijinsia na uchumi DRC
05/03/2025 Duration: 04minShirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limesaidia kujenga utangamano wa kijamii kwa kuboresha maisha kwenye eneo la Walungu jimboni Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Limefanya hivyo kupitia vilabu vya Dimitra ambavyo hupatia wanawake, wanaume na vijana fursa ya uongozi wa kuleta mabadiliko chanya kwa kutatua changamoto zilizo kwenye jamii yao bila hata kuwa tegemezi kwa msaada wa nje. Mradi huu ulitekelezwa kati ya mwaka 2008 na 2023 na sasa tunamulika ni kwa vipi umeleta mafanikio. Sharon Jebichii anaelezea kwenye makala hii kupitia video iliyoandaliwa na FAO.
-
04 MACHI 2025
04/03/2025 Duration: 10minKituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania (TPTC) kilichoko chini ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ/TPDF) kinavyotumia sanaa ya muziki kuelimisha walinda amani kuhusu ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa kingono. Makala hii iliyokusanywa na Florean Kiiza wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kwa kushirikiana na Kapteni Mwijage Francis Inyoma wa JWTZ imechakatwa na Anold Kayanda na inasimuliwa na Flora Nducha.
-
Napenda sana maabara na imenihamasisha kusoma sayansi - Zamzam
03/03/2025 Duration: 02minNchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati. Baadhi ya wasichana wakimbizi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya ni wanufaika wa mpango huu. Sharon Jebiichi na maelezo zaidi.Zamzam Hussein,aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Hagadera. Ni mkimbizi mwenye asili ya Somalia na sasa anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Daadab nchini Kenya akiwa na ndoto ya kuwa daktari. Kupitia mpango huu ambao ni sehemu ya programu ya PROSPECTS ambao ni ushirikiano wa kimataifa unaojumuisha mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ukilenga kuboresha upatikanaji wa elimu, ulinzi wa jamii, na ajira yenye hadhi kwa jamii zinazowakaribisha wakimbizi na watu waliolazimika kuhama makazi yao Zamzam Hussein ameweza kukumbatia sayansi.“Nilikuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Hagadera na nikamaliza elimu yangu mwaka wa 2024. Nilijiunga na shule hiyo Agosti 2021
-
Viongozi wababe, wa kiimla na wenye fedha wanasigina haki za binadamu duniani
03/03/2025 Duration: 02minKwenye kikao cha 58 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachoendellea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa M ataifa, Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani kote akielezea wasiwasi mkubwa kuhusu kudhoofika kwa makubaliano ya kimataifa kuhusu haki za binadamu,na kuonya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Anold Kakayanda na taarifa kamili.Asante Flora katika taarifa yake Türk amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi haki za binadamu na utawala wa sheria ili kuzuia kurudiwa kwa ukatili wa zamani.Moja ya masuala ya dharura yaliyotiliwa mkazo na Türk ni mgogoro wa kibinadamu unhaoendelea huko Gaza. Amelaani uharibifu uliosababishwa na hatua za kijeshi za Israeli dhidi ya mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 yaliyofanywa na Hamas na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina.Türk amesisitiza haja ya kudumisha usit
-
Burundi yahamishia wakimbizi wa DRC eneo salama zaidi
03/03/2025 Duration: 03minMachafuko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) yanaendelea kufurusha watu na wengine wanaamua kukimbilia nchi jirani ikiwemo Burundi. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Burundi limesema wazi kuwa katika wiki mbili za mwezi Februari kuanzia tarehe 14 walipokea wakimbizi zaidi ya 60,000, wengi wakiwa tayari walishafurushwa awali. Kwa waliowasili katika eneo la Kaburantwa nchini Burundi, bado wanahofia usalama. Serikali ya Burundi imetenga eneo lingine salama zaidi na sasa wanahamishiwa huko. Je ni wapi? Assumpta Massoi kwa msaada wa video ya UNHCR Burundi anasimulia zaidi.
-
03 MACHI 2025
03/03/2025 Duration: 11minKaribu jaridani hii leo na mwenyeji wako ni Flora Nducha akikuletea habari kuhusu haki za binadamu, elimu ya STEM kwa wasichana wakimbizi nchini Kenya; Harakati za kuhamishia wakimbizi wa DRC nchini Burundi kuelekea maeneo salama; mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni kwa wanawake na wasichana.Kwenye mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu unaoendelea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani, akionya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Ripoti yake Anold Kayanda.Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.Ripoti yake Sharon Jebiichi.Makala Assumpta Massoi anakupeleka mpakani mwa Burundi na Jamhuri ya Ki
-
Kutana na Celestin Mbaruku mkimbizi mnufaika wa Mpango wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali nchini Kenya
28/02/2025 Duration: 03minKama mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Celestin Mbaruku hakuwa na fursa ya ajira rasmi hadi alipothibitishwa ujuzi wake kupitia mpango wa Serikali ya Kenya wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali, uliotengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO.Kupitia ILO Celestin Mbaruku ni mnufaika wa ufadhili wa PROSPECTS, ushirikiano wa kimataifa unaojumuisha mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ukilenga kuboresha upatikanaji wa elimu, ulinzi wa jamii, na ajira yenye hadhi kwa jamii zinazowakaribisha wakimbizi na watu waliolazimika kuhama makazi yao.Kimakosa, Celestin Mbaruku akiwa nchini mwake DRC alidhaniwa kuwa muasi, akafungwa lakini akamudu kutoroka hadi Kenya.Kabla ya masaibu haya, huko DRC alikuwa Mwalimu anayesimamia nidhamu katika shule alikokuwa anafanya kazi ya lakini kwa kuwa vyeti vyake vilipotea, hata alipovuka kuingia Kenya, hakuwa na uthibitisho wa kiwango cha elimu yake licha ya kuwa ana diploma ya mbinu za ufundishaji.Na hapo ndipo ikabidi achomoe kibin
-
Guterres: Mwezi Mtukufu wa Ramadhani utumike kuleta amani
28/02/2025 Duration: 02minKuelekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwishoni mwa wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe wake wa kutaka kipindi hicho cha takribani siku 30 kitumike kuleta amani na kuongoza kuelekea dunia yenye yenye haki na huruma zaidi. Selina Jerobon na taarifa zaidi.
-
28 FEBRUARI 2025
28/02/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunaangazia migogoro ambayo yameendelee kwa muda mrefu Sudan Kusini, na ujumbe wa Katibu Mkuu ikielekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Makala inatupeleka nchini Kenya, na mashinani nchini Tanzania.Viongozi wa kisiasa wa Sudan Kusini lazima wakabiliane na ukwepaji wa sheria na ufisadi unaochochea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, la sivyo watahatarisha mpito wa kisiasa wa nchi hiyo, imesema Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Sudan Kusini katika ripoti yake iliyotolewa leo.Kuelekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwishoni mwa wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe wake wa kutaka kipindi hicho cha takribani siku 30 kitumike kuleta amani na kuongoza kuelekea dunia yenye yenye haki na huruma zaidi..Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii kutokana na video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, anakupeleka nchini Kenya kukutanisha na mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC am
-
Viongozi wabainika kuwa chanzo cha kutomalizika kwa mzozo nchini Sudan Kusini
28/02/2025 Duration: 02minViongozi wa kisiasa wa Sudan Kusini lazima wakabiliane na ukwepaji wa sheria na ufisadi unaochochea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, la sivyo watahatarisha mpito wa kisiasa wa nchi hiyo, imesema Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Sudan Kusini katika ripoti yake iliyotolewa leo kama anavyoripoti Flora Nducha.
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “Fahari isiyo pari haina heri"
27/02/2025 Duration: 01minKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “FAHARI ISIYO PARI HAINA HERI.”.
-
27 FEBRUARI 2025
27/02/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka nchini DRC ambako leo tunamulika mmoja wa raia aliyerejea makazi yake huko Sake, nje kidogo ya mji wa Goma, jimboni Kivu Kaskazini baada ya waasi wa M23 kutangaza kuwa wakimbizi wote wa ndani lazima warejee vijijini kwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali.Ikiwa ni mwezi mmoja sasa tangu waasi wa M23 watwae mji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kuendelea kutwaa miji mingine huku mamia ya maelfu ya watu wakifurushwa makwao, hii leo mashirika ya Kibinadamu nchini humo yametoa ombi la dola bilioni 2.54 ili kusaidia watu milioni 11 walioathiriwa vibaya na mzozo unaoendelea.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO Dkt. Tedros Ghebreysus ametangaza kuwa ugonjwa wa mpox bado ni tishio la afya ya umma duniani na hivyo nchi lazima ziendelee kuwa makini katika ufuatiliaji, uchunguzi, kinga na matibabu.Na kuelekea Mkutano wa viongozi kuhusu Mifumo ya uzalishaji