Habari Za Un
02 OKTOBA 2025
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:11:08
- More information
Informações:
Synopsis
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ujumbe wa Omon Ukpoma-Olaiya, Kiongozi wa Uwekezaji wa UNCDF kwa Kanda ya Afrika Mashariki, Kusini na Nchi za Kiarabu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi neno la wiki.Haiti, hali ya kibinadamu imefika kiwango cha hatari, amesema Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk. Akihutubia Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Türk amesema Haiti imefika kiwango cha kulipuka kutokana na ukatili na ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu. Amesisitiza kuwa “Tunaweza na lazima kubadili hali hii kwa ajili ya watu wa Haiti,” akiongeza kuwa “bila hatua za haraka hali mbaya zaidi huenda ikaja kwa Haiti na eneo zima.”Tukielekea Mashariki ya Kati huko Gaza, janga la kibinadamiu linaongezeka ambapo mashambulizi yanayoendelea yameathiri vibaya upatikanaji wa chakula na maji. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA, limeripoti kuwa usambazaji wa chakula kilichopikwa kaskazini mwa Gaza umepungua kwa asilim