Habari Za Un

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 8:56:33
  • More information

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • UN: Hali inazidi kuwa tete Gaza huku watu zaidi ya milioni wakiwa hatarini kukosa mlo

    26/03/2025 Duration: 02min

    Watu zaidi ya milioni 1 wako katika hatari ya kukosa chakula endapo misaada haitoruhusiwa kuingia Gaza wakati huu mashambulizi makali ya Israel yakizidisha janga la kibinadamu yameonya leo mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa. Flora Nducha na taarifa zaidi.

  • 26 MACHI 2025

    26/03/2025 Duration: 11min
  • Baada ya kukimbilia Burundi, wakimbizi wa DRC wakubwa na uhaba wa mahitaji muhimu

    26/03/2025 Duration: 02min

    Hali ya kibinadamu ya wakimbizi zaidi ya 100,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, waliokimbilia nchini Burundi kusaka usalama kutokana na mapigano mashariki mwa nchi yao katika katika kipindi cha chini ya miezi mitatu, iliyopita ni ya mashaka, wakati huu ambapo ufadhili unazidi kukumbwa na mkwamo, wakikabiliwa na uhaba wa huduma kama chakula, huku kukiwa na pengo la ufadhili. Je ni madhila yapi?  Sharon Jebichii anafafanua zaidi kupitia video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.

  • 25 MACHI 2025

    25/03/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana, tunamsikia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake, Mkutano wa Beijing Bi. Gertrude Mongella.Hapa New York, Umoja wa Mataifa leo umetoa wito wa kuachiliwa kwa wafanyakazi wake wanaoshikiliwa kote ulimwenguni ambao wamejikuta matatani wakati wakiwahudumia watu walio katika hatari, huku wakihatarisha usalama wao binafsi kwa kukabiliwa na vitisho vya kutekwa nyara, vurugu, unyanyasaji, na kifungo katika maeneo yenye migogoro na majanga.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kuhusu vifo vya watoto imeonya kwamba miongo ya maendeleo katika kupunguza vifo vya watoto na watoto wachanga wakati wa kuzaliwa yako hatarini kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili. Idadi ya vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano ilipungua hadi watoto milioni 4.8 mwaka 2023, huku vifo vya wakati wa kuzaliwa vikiendelea kubaki

  • Wanawake wamefanya mengi lakini hayajarekodiwa - Dkt. Reuben CSW69

    24/03/2025 Duration: 03min

    Rekodi ni chache sana ya vitu ambavyo wanawake wamefanya hapa duniani, anasema Dkt. Rose Reuben, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania anapozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa wakati wa Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69, jijini New York, Marekani.Mkutano huu muhimu kuhusu wanawake umefanyika kuanzia tarehe 10 hadi 21Machi 2025 na kuhudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka kote duniani naye Dkt. Rose Reuben akiwa mmoja wao.Kiongozi huyu wa waandishi wa habari nchini Tanzania anaona kwamba kuna hatua nyingi zimepigwa  katika kipindi cha miaka 30 tangu kuwekwa kwa Azimio la Beijing ili kumkomboa mwanamke lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya.“Na hii kazi sipendi kujilaumu sana kwamba je, hakuna kitu ambacho kimefanyika?! Mambo yamefanyika mengi lakini masuala ya kijamii hayamaliziki kwa usiku mmoja kwasababu kila unapoamka jamii inabadilika kwa namna nyingine. Kwa hiyo tukitazama kwa mtazamo huo tunaona kwamba kuna kazi

  • UNAIDS: Kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani ni janga kubwa kwa vita dhidi ya ukimwi na chachu ya vifo

    24/03/2025 Duration: 02min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS leo limeonya kwamba kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani sio tu janga kwa vita dhidi ya gonjwa hilo bali ni chachu ya vifo na ongezeko la maambukizi mapya. Flora Nducha amefuatilia onyo hilo lililotolewa leo mjini Geneva Uswisi na Mkurugenzi mtendaji wa UNAUDS Winnie Byanyima alipozungumza na waandishi wa habari.

  • 24 MACHI 2025

    24/03/2025 Duration: 12min

    Hii leo jaridani tunaangazia hatari za usitishwaji wa misaada kutoka marekani kwa waathirika wa viruzi vya Ukimwi, na ujumbe wa washiriki wa Mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana. Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS leo limeonya kwamba kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani sio tu janga kwa vita dhidi ya gonjwa hilo bali ni chachu ya vifo na ongezeko la maambukizi mapya. Flora Nducha amefuatilia onyo hilo lililotolewa leo mjini Geneva Uswisi na Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS Winnie Byanyima alipozungumza na waandishi wa habari.Wakati Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani ulioleta pamoja wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa  pamoja na mashirka yasiyo ya kiserikali(NGOs) ulikunja jamvi      ijumaa tarehe 21 Machi wiki jana tulipata kuzungumza na wawakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Forum for Women Democracy Development and Justice, FODAJ amba

  • FODAJ CSW69: Vita dhidi ya dhulma kwa wanawake na wasichana

    24/03/2025 Duration: 02min

    Wakati Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani ulioleta pamoja wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa  pamoja na mashirka yasiyo ya kiserikali(NGOs) ulikunja jamvi  ijumaa tarehe 21 Machi wiki jana tulipata kuzungumza na wawakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Forum for Women Democracy Development and Justice, FODAJ ambalo linasaidia wasichana na wanawake waathirika wa ukatili wa kijinsia katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Sharon Jeichii anaeleza waliochokizungumzia.

  • Zanzibar tumetekeleza kwa vitendo azimio la Beijing: Waziri Riziki Pembe

    21/03/2025 Duration: 05min

    Wakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW69 ukifikia ukingoni mshiriki kutoka Zanzibar Tanzania ameweleza Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili kwamba Zanzibar imepiga hatua kubwa katika usawa wa kijinsia na utekelezaji kwa vitendo matakwa ya Azimio la Beijing la usawa wa kijinsia na hatua. Je wametekeleza vipi na hatua gani walizopiga? Ungana nao katika mahojiano haya.

  • Ukiwekeza kiuchumi kwa mwanamke basi umewekeza katika jamii: Janet Mbene mshiriki CSW69

    21/03/2025 Duration: 05min

    Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani CSW69 unakunja jamvi leo hapa makao makuu ya Umoja wa  Mataifa New York Marekani baada ya mjadala wa wiki mbili kutathimini hatua zilizopigwa na changamoto zilizosalia miaka 30 baada ya azimio la Beijing la usawa wa kijinsia nah atua za utekelezaji. Flora Nducha amebahatika kuzungumza na mmoja wa wakishiri wa mkutano huo kutoka asasi za kiraia nchini Tanzania

  • IFAD yawaepusha vijana wa kike 5 na kazi za ndani na kuwajengea stadi za kilimo biashara Senegal

    21/03/2025 Duration: 02min

    Tukiwa bado ndani ya mwezi wa Machi, unaotambuliwa kuwa ni mwezi wa wanawake tunakwenda nchini Senegal ambako huko wasichana waliokuwa wakifanya kazi za ndani, wamewezeshwa na Umoja wa Mataifa na sasa ni wakulima na wanatumia stadi za upigaji na utengenezaji video za mtandaoni kuelimisha jamii kuhusu kilimo chenye tija. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

  • 21 MACHI 2025

    21/03/2025 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW69 unafikia tamati hii leo Machi 21 hapa katika makao makuu, na wakulima wanawake nchini Senegal. Mashinani inatupeleka nchini Tanzania kumulika mradi wa maji.Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW69 unafikia tamati hii leo Machi 21 hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Bi. Gertrude Mongella, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa wanawake maarufu kama Mkutano wa Beijing uliofanyika mnamo mwaka 1995, hivi tunavyozungumza, pamoja na umri wake mkubwa ameshirikia karibia vikao vyote vya mkutano huu wa CSW69 ambao pia ulikuwa unaangazia utekelezaji wa maazimio yaliyowekwa miaka 30 iliyopita chini yake mama Mongella.Tukiwa bado ndani ya mwezi wa Machi, unaotambuliwa kuwa ni mwezi wa wanawake tunakwenda nchini Senegal ambako huko wasichana waliokuwa wakifanya kazi za ndani, wamewezeshwa na Umoja wa Mataifa na sasa ni wakulima na wanatumia stadi za upigaji na ut

  • Wanaume 'wapenzi wetu' msiwe na hofu na sisi - Bi. Gertrude Mongella

    21/03/2025 Duration: 01min

    Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW69 unafikia tamati hii leo Machi 21 hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Bi. Gertrude Mongella, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa wanawake maarufu kama Mkutano wa Beijing uliofanyika mnamo mwaka 1995, hivi tunavyozungumza, pamoja na umri wake mkubwa ameshirikia karibia vikao vyote vya mkutano huu wa CSW69 ambao pia ulikuwa unaangazia utekelezaji wa maazimio yaliyowekwa miaka 30 iliyopita chini yake mama Mongella.Nilipokutana naye nimemuuliza swali hili la kichokozi.Mazungumzo zaidi kati yangu na Mama Gertrude Mongella yatakujia katika vipindi vyetu vijavyo hivi karibuni.

  • Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa maneno "Ashiraf, Janabi, gayagaya, kiti cha marimba na kiti cha msaji"

    20/03/2025 Duration: 59s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “Ashiraf, Janabi, gayagaya, kiti cha marimba na kiti cha msaji” 

  • 20 MACHI 2025

    20/03/2025 Duration: 12min

    Hii leo jaridani katika mada kwa kina tunajikita katika mkutano CSW69 ambao umebakiza siku moja tu, kesho Machi 21 unakunja jamvi, na tunamsikia Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Tanzania, Waziri Riziki Pembe kutoka Zanzibar na Profesa Smile Dzisi, Mkugenzi wa Shirika la “I believe Global” kutoka Ghana.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amesema kukata ufadhili kwa mashirika yanayotoa huduma za kibinadamu kunasababisha janga la uwajibikaji. Kupitia taarifa iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na UNHCR, Bwana Grandi amesema kukata ufadhili kunaweka hatarini maisha ya mamilioni ya watu na madhara yake kwa watu wanaokimbia majanga, yatakuwa makubwa zaidi na yataonekana wazi ikiwemo wanawake na watoto wa kike kukosa huduma zitokanazo na kubakwa.Leo ni siku ya furaha duniani maudhui yakimulika umuhimu wa watu kusaidiana na kujaliana katika masuala mbalimbali ikiwemo chakula. Ripoti mpya ya wadau wa UN iliyozinduliwa leo imeonesha kuwa nchi ye

  • Lengo langu ni kuona wasichana wadogo wanashiriki kwa wingi CSW - Zahra Salehe ICCAO

    19/03/2025 Duration: 03min

    Katika makala Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ICCAO kutoka Tanzania, Zahra Salehe, mshiriki mwingine kutoka Tanzania anayehudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW69 unaoendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York Marekani. 

  • Haki za wanawake na wasichana lazima zizingatiwe na zipewe kipaumbele - Ochieng CSW69

    19/03/2025 Duration: 02min

    Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa shirika la slums foundation lililoko  jijiniNairobi, Kenya naye anashiriki mkutano huu wa CSW69 na ameueleza Sharon Jebichii wa Idhaa hii  kilichomleta hapa, matarajio yake na ushauri kwa wasichana na wanawake.

  • 19 NACHI 2025

    19/03/2025 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu, na yaliyojiri hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa mkutano wa 69 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW69.Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu yameongezeka kwa viwango vya kutisha mwaka 2024, na baadhi ya athari hasi zinaweza kuwa zisizoweza kurekebishwa kwa karne nyingi – kama si milenia, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, (WMO).Tukirejea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa shirika la slums foundation lililoko  jijiniNairobi, Kenya naye anashiriki mkutano huu wa CSW69 na ameueleza Sharon Jebichii wa Idhaa hii  kilichomleta hapa, matarajio yake na ushauri kwa wasichana na wanawake..Makala Flora Nducha wa Idhaa hii anazun

  • WMO: Joto likizidi kuongezeka duniani, mwaka 2024 wathibitishwa kuwa ulikuwa wa joto zaidi

    19/03/2025 Duration: 01min

    Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu yameongezeka kwa viwango vya kutisha mwaka 2024, na baadhi ya athari hasi zinaweza kuwa zisizoweza kurekebishwa kwa karne nyingi – kama si milenia, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, (WMO). Anold Kayanda na maelezo zaidi.

  • 18 MACHI 2025

    18/03/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika elimu ya mtoto wa kike kama moja ya nguzo muhimu katika jamii ukizingatia malengo endelevu ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na sauti za mashinani.Viongozi wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali mashambulizi ya anga ya Israel huko Ukanda wa Gaza na kutoa wito kwa kusitisha uhasama mara moja. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonesha mshtuko na wasiwasi mkubwa kuhusu mashambulizi hayo akitoa wito kwa pande zote kuheshimu usitishaji mapigano, kurejesha misaada ya kibinadamu bila vikwazo, na kuhakikisha kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa mateka waliobaki.Ghasia zinazoendelea katika kaunti za Nasir, Ulang, na Baliet, Jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini zimeathiri vibaya jamii za eneo hilo na shughuli za kibinadamu, na kusababisha watu takriban 50,000 kukimbia makazi yao tangu mwishoni mwa mwezi Februari amesema Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini S

page 3 from 5