Habari Za Un
Harakati za UN na serikali ya Uganda kukabili tabianchi huko Karamoja
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:02:55
- More information
Informações:
Synopsis
Karamoja, eneo la kaskazini mashariki mwa Uganda, linakabiliwa na changamoto kubwa za tabianchi kama vile ukame wa mara kwa mara na milipuko ya magonjwa ya mimea na mifugo, hali inayotishia uhakika wa chakula. Kupitia mradi wa PROACT, mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), na Mpango wa chakula Duniani (WFP) pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uganda kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya, EU, wameshirikiana katika kuimarisha mifumo ya kushughulikia mabadiliko ya kiikolojia na kijamii. Anold Kayanda na maelezo zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda) Video iliyoandaliwa na FAO inaanza ikionesha wana jamii katika eneo la Karamoja wanavyojihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kilimo na ufugaji licha ya changamoto za tabianchi. Dustan Balaba Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Uganda anaeleza kuhusu mradi huu mpya akisema,"Wadau wameweza kuhakikisha kwamba kuna maendeleo ya haraka katika upatikanaji wa taarifa na tunatumia maendeleo ya kiteknolojia kwa m