Synopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodes
-
Maoni ya waskilizaji wetu Juma hili
31/05/2025 Duration: 09minKila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi ya kuchangia mada yoyote iwe kila uliskia kwenye habari zetu au kile kinachoendelea hapo ulipo. Skiza maoni ya mskilizaji.
-
Uganda : Ombi la Msamaha wa rais Museveni ni la kweli
29/05/2025 Duration: 09minLeo shaba yetu inalenga taifa la Uganda ambapo rais Yoweri #Museveni pamoja na mkewe wameomba raia wa nchi hiyo msamaha kwa mabaya yote ambayo serikali yao imetekeleza kwa miaka 39. Je, unafikiri kauli ya Rais Museveni na Mama Janet kuomba msamaha ni ya kweli au ni ya kisiasa?Skiza maoni ya mskilizaji wetu.
-
EAC : Je wanachama wana cha kujivunia
28/05/2025 Duration: 09minKatika makala haya shaba yetu inalenga jumuia ya Africa mashariki, tumekuuliza mskilizaji je unahisi una chochote cha kujivunia kuwa mwanachama wa jumuiya ya Africa Mashariki. Skiza maoni ya mskilizaji wetu.
-
Africa: Ina lolote cha kujivunia
27/05/2025 Duration: 09minUmoja wa Afrika imesherekea siku ya kiafrika, kuadimisha kuundwa kwa Umoja wa Afrika, kipindi hiki nchi ya Uganda nayo ikisitisha ushirikiano wake wa kijeshi na taifa la Ujerumani. Kuna chochote bara la Afrika linaweza kujivunia?Ndilo swali tumekuuliza, skiza makala haya kuskia maoni ya waskilizaji.
-
DRC: Kabila kuondolewa kinga je ni sahihi
26/05/2025 Duration: 09minKwenye makala haya tunajadili kilichotokea nchini DRC ambapo bunge la seneti lilimuondolea kinga ya kutoshtakiwa rais wa zamani, Joseph Kabila, hatua ambayo sasa inatoa nafasi kwa mahakama ya kijeshi kumshtaki kiongozi huyo kwa tuhuma za uhaini. Unazungumziaje hatua hii ya seneti, unadhani ilikuwa sahihi?Ndio swali tumekuuliza?skiza maoni ya baadhi ya waskilizaji.
-
Maoni ya waskilizaji kuhusu habari zetu juma hili
23/05/2025 Duration: 09minIlivyo ada kila siku ya ijumaa rfi Kiswahili hukiupa nafasi kuchangia chochote kile, maana yake nini? unachangia chochote kile, ulichoskia kwenye habari zetu au kile kinachoendelea hapo ulipo. Skiza makala haya kuelewa zaidi.
-
Mazungumzo ya Kigali na Washington kuhusu Rwanda kuwapokea wahamiaji kutoka Marekani
22/05/2025 Duration: 10minLeo hii tunaangazia Mazungumzo kati ya nchi ya Rwanda na Marekani kuhusu Kigali kuwapokea wahamiaji haramu watakaofukuzwa kutoka Washington. Unazungumziaje mazungumzo haya sawia na kauli ya mashirika ya Kimataifa ya kutetea haki za binadamu yakiongozwa na Amnesty International, yanayosema mpango huo utakiuka haki za wakimbizi?Skiliza kauli mbalimbali katika makala ya leo.
-
Uganda yapitisha mswada kuruhusu raia kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi
21/05/2025 Duration: 09minWabunge wa upinzani hata hivyo walisusia kikao kilichopitisha mswada huo kwa haraka. Wanasiasa wa upinzani wanadai mswada huo unawalenga wakosoaji wa rais Yoweri Museveni
-
Kauli ya rais wa Tanzania Samia Suluhu kuwazuia wanaharakati wa nchi zingine
20/05/2025 Duration: 09minLeo tunaangazia ,hatua ya Tanzania kuwazuia Mawakili, wanaharakati wa haki za binadamu kutoka nchini Kenya, akiwemo Jaji Mkuu mstaafu Willy Mutunga waliokwenda kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi mkuu wa upinzani Tundu Lissu. Rais Samia Suluhu Hassan, amesema serikali yake haitaruhusu wanaharakati wa kigeni kuingia nchini Tanzania na kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.
-
Nini kifanyike kumaliza vita vinavyoendelea Sudan,Ukraine na Gaza
19/05/2025 Duration: 10minViongozi wa dunia, wameendelea kutoa wito wa amani kwenye nchi za Sudan Ukraine na Gaza hizo, ambako vita vimesababisha vifo vya maelfu ya raia na wengine kuwa wakimbizi. Hata hivyo licha ya wito huu, mapigano yameendelea kuripotiwa.
-
-
-
Maoni ya waskilizaji kuhusu vipindi vyetu juma hili
09/05/2025 Duration: 09minJuma hili waskilizaji wetu walikuwa na maoni haya kuhusu taarifa zetu
-
Je kuna hofu ya kutokea kwa vita vya tatu vya dunia
08/05/2025 Duration: 10minKatika makala haya tunajadili athari ya vita vya ukraine na Urusi na sasa tishio la vita nyingine kati ya India na Pakistan. Je ni shara ya kutokea kwa vita vya pili vya dunia ? ndilo swali tumekuuliza. Skiza baadhi ya maoni ya waskilizaji.
-
News Zealand kudhibiti mitandao ya kijamii kwa watoto
07/05/2025 Duration: 09minShaba ya makala haya inalenga news Zealand ambapo serikali inapendekeza marufuku ya matumizi ya mitandao kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 16, lengo likiwa kuwakinga dhidi ya athari za mitandao. Njia gani wazazi wa kiafrika wanaweza kuwalinda watoto na mitandao ya kijamii? Ndilo swali tumeuuliza na haya hapa baadhi ya maoni yako, skiza makala haya.
-
Dunia uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari
05/05/2025 Duration: 09minLeo mada yetu inajikita kwa siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari, ambapo Umoja wa Mataifa umesema licha ya baadhi ya nchi kupiga hatua katika ulinzi wa wanahabari, hofu ya uhuru wa habari kuendelea kuminywa inaendelea kutanda. Mwaka jana jumla ya wanahabari 82 walipoteza maisha wakitekeleza majukumu yao. Tuambie nchini mwako vyombo vya habari viko huru? Haya hapa baadhi ya maoni yako, skiza makala.
-
-
-
Mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa kanisa katoliki duniani
28/04/2025 Duration: 10minKwa sasa macho yakiwamulika makadinali 135 watakaochagua papa mpya ndani ya siku chache zijazo, mjadala kuhusu Papa kutoka Afrika ukishamiri.Mchakato wa kumchagua p
-
Joseph Kabila adaiwa kurejea DRC kupitia Goma
21/04/2025 Duration: 09minJuma lililopita ripoti ambazo hazijathibitishwa rasmi zilieleza kuwa rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila alirejea nchini Mwake kupitia mji wa Goma unaokaliwa na waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda. Hata hivyo hatua yake imeifanya serikali ya Kinshasa, kusimamisha shughuli zote za chama chake cha PPRD, ikikituhumu kushurikiana na waasi hao.Unazungumziaje kurejea kwa rais Kabila?Ndilo swali tumekuuliza katika makala haya.Skiza maoni ya mskilizaji.