Habari Za Un
14 JULAI 2025
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:09:51
- More information
Informações:
Synopsis
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya malengo ya maendeleo endelevu, na mradi wa uvuvi unaosaidia kupunguza migogoro Ituri DRC. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu la Maendeleo Endelevu, HLPF la mwaka huu wa 2025 limeanza leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo wadau kutoka katika nyanja mbalimbali duniani wanakutana kujadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.Kutoka msituni kupigana upande wa waasi hadi kuingia ziwani na kuwa mtaalamu wa ufugaji wa samaki, ndio simulizi tunayopata kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, simulizi ya matumaini kwa mustakabali wa jamii iliyogubikwa na vita kila uchao.Katika makala tunakupeleka mkoani Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambako kuelekea siku ya kimataifa ya vijana na stadi hapo kesho Julai 15, Sabrina Said anazungumza na mmoja wa vijana anayetumia majukwaa ya kidijitali kutoa elimu ya &