Habari Za Un

15 JULAI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika juhudi za kinamama wajawazito na wanao kuambatana wakihudhuria kliniki kwa ajili ya mimbasalama. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Takribani wapalestina 900 wameuawa katika wiki za hivi karibuni huko Ukanda wa Gaza, eneo linalokaliwa kimabavu na Israeli. wakihaha kupokea chakula. Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Thameen Al-Kheetan amewaeleza waandishi wa habari Geneva, Uswisi kuwa watu 674 kati yao waliuawa wakiwa kwenye maeneo ya Mfuko wa Kiutu wa Gaza, (GHF) unaoendeshwa na Israeli na Marekani.Wakati huo huo Bwana Al-Kheetan amezungumzia mauaji yanayoendelea Ukingo wa Magharibi ikiwemo Yerusalemu Mashariki akisema, “muathirika mdogo zaidi ni Laila Khatib mwenye umri wa miaka miwili. Alipigwa risasi ya kichwa na jeshi la Israeli akiwa nyumbani kwao kijijini Ash-Shuhada.”Na leo ikiwa siku ya kimataifa ya stadi kwa vijana Sangheon Lee, Mkurugenzi wa Ajira na Sera katika Shirika la Umoja wa M