Habari Za Un

Kujituma na kutokata tamaa ndio siri ya kufanikiwa kwenye mafunzo kwa vitendo UN - Sarah Nshoka

Informações:

Synopsis

Kutoka Dar es Salaam hadi Geneva, na sasa New York. Ni safari ya kujifunza, kujaribu na kufanikiwa. Kwa vijana wengi barani Afrika, Umoja wa Mataifa huonekana kuwa ndoto isiyowezekana. Lakini kijana huyu kutoka Tanzania anathibitisha kuwa kwa nia thabiti na bidii, ndoto hiyo inaweza kuwa kweli. Kupitia programu ya mafunzo kwa vitendo ya Umoja wa Mataifa, amejifunza mengi kuhusu utawala, maendeleo na kujenga ujasiri wa kushiriki katika kazi za kimataifa. Sarah Nshoka alipata fursa kuzungumza na Shraon Jebichii katika makala hii.