Habari Za Un

18 JULAI 2025

Informações:

Synopsis

Jaridani leo naangazia hafla ya Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela katika makao makuu ya Umoja wa mataifa na ujumbe wa washindi wa Tozo ya Mandela. Makala tunakwenda nchini Angola na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Umoja wa Mataifa leo katika makao yake makuu jijini New York, Marekani, umeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela kwa heshima ya maisha na urithi wa shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, nchini Afrika Kusini, Nelson Rolihlahla Mandela, al maarufu Madiba. Assumpta Massoi amefuatilia na kutuandalia taarifa ifuatayo.Mapema kabla ya kushiriki hafla hii ya utoaji wa tuzo katika siku hii ya kimataifa ya Nelson Mandela hapa New York, Kennedy Odede alizungumza na Zipporah Musau wa Umoja wa Mataifa.Katika makala Sabrina Saidi anatupeleka huko Manispaa ya Caluquembe jimboni Hiula, Kusini Magharibi mwa Angola, Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa kushirikiana na mamlaka za mitaa, limeongeza juhudi za ushirikishwaji wa jamii na afua za afya ya umma, ili kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu un