Habari Za Un

WHO na mamlaka za mitaa waungana kupambana na Kipindupindu Caluquembe nchini Angola

Informações:

Synopsis

Huko Manispaa ya Caluquembe jimboni Hiula, Kusini Magharibi mwa Angola, Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa kushirikiana na mamlaka za mitaa, limeongeza juhudi za ushirikishwaji wa jamii na afua za afya ya umma, ili kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu unaoendelea nchini humo. Lengo kuu likiwa ni kuongeza uelewa kuhusu kipindupindu kupitia mikutano ya jamii, jumbe za afya ya umma, na ujenzi wa miundombinu muhimu kama vile vyoo na vituo vya kupata maji safi ya kunywa ndani ya manispaa. Sabrina Saidi amefuatilia na kueleza zaidi katika makala hii.