Habari Za Un
21 JULAI 2025
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:09:35
- More information
Informações:
Synopsis
Jaridani leo tunaangazia msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na uhakika wa chakula nchini Uganda. Makala tunaangazia mradi wa kulinda mazingira na kazi za kujitolea. Mashinani inamulika utayari wa nchi ya Nigeia kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, kupitia Apu yake ya kidigitali Gawa Chakula au ShareTheMeal, limeingia ushirikiano na Apu maarufu huko Mashariki ya Kati iitwayo Careem na kuzindua kampeni ya kuchangisha msaada wa dharura kwa watu wanaokumbwa na njaa katika eneo la Gaza na Ukingo wa Magharibi maeneo yanayokaliwa kimabavu na Israeli.Licha ya changamoto za ufadhili, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Uganda linasisitiza umuhimu wa usafirishaji katika kutoa msaada wa chakula. Sahir Aslam, Mkuu wa Idara ya Ugavi ya WFP Uganda, akizungumza kutokea huko huko Uganda katika maghala ya shirika hilo anafafanua kila kilomita moja ambayo msaada wa chakula wa WFP unasafiri.Katika makala Assumpta Massoi