Habari Za Un

22 JULAI 2025

Informações:

Synopsis

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika SDG17 katika mazungumzo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa na idhaa hii hivi karibuni hapa New York.  Pia tunakuletea mutasari wa habari na mashinani.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo jijini Geneva Uswisi amekemea amri za hivi karibuni za Israel za kuwahamisha watu Gaza, zilizoambatana na mashambulizi makali katika eneo la kusini-magharibi mwa Deir El Balah na kwamba zimeongeza machungu zaidi kwa mateso ya Wapalestina wenye njaa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP) limeeleza leo kuwa kutokana na upungufu wa ufadhili, mamilioni ya watu Sudna Kusini wako hatarini kukosa msaada wa chakula. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa WFP ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Carl Skau, ambaye hivi karibuni ametembelea Sudan Kusini anasema, "Kote Sudan Kusini, takriban watu milioni 8 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, wengi wao wakitegemea