Habari Za Un
04 Agosti 2025
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:09:59
- More information
Informações:
Synopsis
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mlipuko wa kipindupingu nchini Sudan. Makala tunafuatilia ziara ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kazakhstan na mashinani tunamulika unyonyeshaji Sudan Kusini.Simulizi za huzuni, majonzi na kukata tamaa zinaendelea kila uchao huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel hasa wakati huu ambapo raia wanaokwenda kusaka chakula wanakumbwa na mashambulizi yanayosababisha vifo. Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa na mamia kadhaa walijeruhiwa katika siku mbili pekee Wakisaka chakula.Zaidi ya watoto 640,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wapo hatarini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huko Kaskazini mwa Darfur, nchini Sudan.. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka Asia ya Kati ambako Umoja wa Mataifa na Kazakhstan wamesaini makubaliano ya Kazakhstan kuwa mwenyeji wa Kituo cha Kikanda cha Umoja wa Mataifa cha Malengo ya Maendeleo Endelevu kw