Habari Za Un

12 AGOSTI 2025

Informações:

Synopsis

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Bahrain, wadau kwa kushirikiaa na ofisi ya Uwekezaji na Uendelezaji Teknolojia, ITPO ya shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO wanachukua hatua kuondolea wanawake umaskini kwa kuimarisha talanta walizonazo. Mengine ni kama yafuatayo..Leo ni siku ya Kimataifa ya vijana duniani maadhinisho yanafanyika jijini Nairobi nchini Kenya chini ya ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewatumia vijana ujumbe maalum akisema “Kwa kijana: Sauti yako, mawazo yako na uongozi ni muhimu.”Je, vijana wanasemaje kuhusu siku hii? Kutoka Dar es Salaam nchini Tanzania, Sabrina Saidi wa Idhaa hii amezungumza na baadhi yao.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani WFP limepokea zaidi ya dola milioni 2 kutoka Japan kwa ajili ya msaada wa chakula nchini Malawi. Kwa msaada huu WFP inatarajia kusambazana tani 1970 za mahindi katika msimu wa mwambo kwa mwaka 202