Habari Za Un

02 MEI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari Mei 3 tukikuletea ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu umuhimu wake. Pia tunamulika hali ya msaada wa kibinadamu nchini Sudan.Kuelekea siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari Mei 3, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema waandishi wa habari wanakabiliwa na hatari kila uchao huku teknolojia mpya ya akili mnemba au AI ingawa licha ya manufaa nayo pia inaibua hatari mpya kwenye uhuru wa kujieleza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP) tayari limeanza usambazaji wa chakula katika maeneo mbalimbali ya Sudan ambako watu wanakabiliwa na jaa huku wengine wakilazimika kuhama kambi moja hadi nyingine.Makala inamulika siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani itakayoadhimishwa kesho Jumamosi Mei 3 ambayo mwaka huu ikijikita na athari za Akili Mnemba au AI katika uhuru wa habari za vyombo vya habari. Ili kufahamu AI inavyoleta mabadiliko katika vyombo vya habari hususan Afrika Mashariki ambako pia