Habari Za Un

05 MEI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya wakunga na kazi zao muhumi, na mafunzo ya jerahani kwa wakimbizi wa ndani nchini DRC. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakwenda Gaza.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wakunga, tunakwenda nchini Tanzania kummulika mkunga ambaye alinusuru maisha ya wajawazito wawili wakati wa mafuriko makubwa ya Novemba 2023 wilayani Hanang, mkoani Manyara, kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ikiwa ni ushuhuda wa majukumu mazito yanayokumba wakunga.Wanawake 125 katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kigonze, karibu na Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ghasia huripokiwa mara kwa mara, sasa wana matumaini mapya ya kujikwamua kiuchumi baada ya kujiunga na mradi wa mafunzo ya kushona nguo unaofadhiliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO).Makala Assumpta Massoi anamulika uzinduzi wa mtandao wa Mashirika ya Manusura wa Ugaidi duniani,  VoTAN&n