Habari Za Un
UNEP: Licha ya taarifa za ongezeko la gesi ya methane hatua zinazochukuliwa ni kidogo
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:02:05
- More information
Informações:
Synopsis
Mkutano wa 29 wa mkataba wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi COP29 unaofanyika Baku Aberbaijana leo umejikita na ongezeko la gesi ya methane ambayo kwa kiasi kikubwa inachangiwa na shughuli za binadamu na nini kifanyike kuidhibiti. FKulingana na ripoti iliyozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa wa mazingira UNEP katika mkutano huo, mfumo wa teknolojia ya hali ya juu ambao unatambua uvujaji mkubwa wa gesi ya methane umewasilisha tarifa 1,200 kwa serikali na makampuni katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, lakini ni asilimia moja tu ya taarifa hizo ndizo zilizofanyiwa kazi.Ripoti hiyo mpya iliyopewa jina “Jicho kwenye methane: Haionekani lakini inashuhudiwa” inasema licha ya ahadi zilizotolewa chini ya makubaliano ya ahadi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi ya methane kwa asilimia 30 ifikapo 2030 hatua zinazochukuliwa hazitoshelezi kupunguza gesi hiyo.Ripoti imeangazia tahadhari za methane kutoka kwenye Mfumo wa Tahadhari na hatua dhidi ya Methane