Habari Za Un

Walinda amani wa UN kutoka Tanzania wasaidia watoto yatima huko Beni, DRC

Informações:

Synopsis

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mapigano kati ya jeshi la serikali, FARDC na vikundi vilivyojihami, yamesababisha vifo na hata watu kufurushwa makwao. Watoto wamesalia yatima na hawana walezi. Vituo vya kulea watoto yatima vimebeba jukumu la kuwatunza, lakini navyo viko taabani. Walinda amani wa Umoja wa Mataifa, kutoka Tanzania, TANZBATT-11 wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO waliguswa na kuamua kujiongeza na kuwasilisha msaada kwa watoto hao. Afisa Habari wa TANZBATT-11 Kapteni Fadhillah Nayopa anasimulia kile walichofanya.