Synopsis
Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.
Episodes
-
Programu za kufunza watu wazima kusoma na kuandika
21/11/2025 Duration: 05minMmoja kati ya Waaustralia watano, au takriban watu wazima milioni tatu, wana kiwango cha chini cha ujuzi wa kusoma na kuandika au hesabu - na hii inaweza kuwa na athari kubwa katika jinsi watu wanavyoweza kushiriki maisha ya kila siku. Programu zimewekwa kote nchini kusaidia watu kuboresha ujuzi wao na kufikia malengo yao ya maisha. Ikiwemo moja huko Tasmania, ikiwasaidia watu wazima kuwa tayari kwa kazi.
-
Watu wa asili kwenye hatihati ya kutoweka Brazil
18/11/2025 Duration: 08minShirika lisilo la faida linasema karibu nusu ya jamii za Wenyeji wanaoishi mbali na ulimwengu wanakabiliwa na kutoweka ndani ya muongo kutokana na ukataji miti, uchimbaji wa madini na utalii. Survival International wanasema wanataka ulimwengu - hususan serikali na viwanda - kutambua na kushughulikia tatizo hili kama dharura ya kimataifa.
-
Uzalishaji wa Net Zero nchini Australia
18/11/2025 Duration: 08minMuungano umeidhinisha rasmi kuondoa lengo la kutofikia uzalishaji wa gesi chafu katika mkutano wa chumba cha chama huko Canberra. Zaidi ya hayo, Liberals na Nationals wamefunua mpango wa kuondoa mabadiliko ya tabianchi kutoka kwenye orodha ya malengo ya mdhibiti wa nishati ya kitaifa, huku wakiapa kuendelea kupunguza uzalishaji kwa kufuatilia maendeleo ya nchi nyingine.
-
Maumivu ya wanawake kutiliwa maanani zaidi
14/11/2025 Duration: 08minSerikali ya Victoria imetoa ripoti ya mwisho ya uchunguzi kuhusiana na uzoefu wa wanawake katika suala la maumivu - na ni taarifa inayosumbua kusoma. kutokana na uzoefu wa wanawake na wasichana 13,000, ripoti hiyo imebaini mapengo katika huduma za afya kwa jinsia, upendeleo katika matibabu, ubaguzi wa kijinsia, na hisia za kupuuzwa au kutopingwa na wataalamu wa afya zinazoenea katika mfumo wa afya wa Victoria.
-
Maandamano ya kikundi cha NSN uliwezaje kuruhusiwa kufanyika
14/11/2025 Duration: 08minMaandamano ya neo-Nazi mbele ya bunge la New South Wales yamezua mshtuko katika jamii za Kiyahudi na za tamaduni mbalimbali huko Sydney. Serikali ya jimbo hilo imekashifiwa baada ya kufichuliwa kwamba tukio hilo liliendelea na idhini kutoka kwa Polisi wa New South Wales. Je, ni vipi maandamano haya ya neo-Nazi yalipewa kibali cha kufanyika mwanzoni?
-
Mazungumzo kuhusu African Youth Summit 2025
14/11/2025 Duration: 11minMkutano wa kwanza wa African Youth Summit uliandaliwa na kufanyika mwaka huu, na mratibu wa vijana aliyehudhuria anajiunga nasi kuzungumzia mada ya mkutano huo.
-
Idadi ya watoto wa mataifa ya kwanza gerezani yazua tashwishi
11/11/2025 Duration: 08minSerikali ya majimbo na maeneo nchini Australia zitachunguzwa kama sehemu ya uchunguzi wa bunge kuhusu matokeo na athari za kifungo kwa vijana. Kati ya maswala ya kuzingatia katika uchunguzi huu ni Kuzidishwa kwa kufungwa kwa watoto wa Mataifa ya Kwanza.
-
Serikali kudhibiti mitandao ya kijamii kuanzia desemba
11/11/2025 Duration: 06minMtandao wa Reddit na jukwaa la Kick zitaongezwa kwenye majukwaa yanayohitajika kuzuia watumiaji walio na umri chini ya miaka 16, sheria mpya zitakapoanza kutekelezwa mwezi Desemba. Marufuku ya Australia ya mitandao ya kijamii kwa watoto chini ya miaka 16, ambayo inajumuisha majukwaa nane kuu, inategemea tathmini zinazoendelea za eSafety ambazo zinaweza kufafanua kati ya huduma za mitandao ya kijamii, ujumbe, na michezo, kuelezea ni kwanini majukwaa kama Steam na Twitch hayakujumuishwa. Wakati serikali ilihakikishiwa na Roblox kwamba wataanzisha teknolojia za kuthibitisha umri ili kupunguza tabia za uwindaji wa watoto, watetezi wa haki za kidigitali wanatahadharisha kwamba marufuku haya yanaweza kuhamasisha watoto kutumia majukwaa madogo yasiyo na uangalizi ambapo wanaweza kukumbana na madhara makubwa zaidi.
-
Viza ya milioni moja kutolewa nchini Australia
11/11/2025 Duration: 07minAustralia inatarajia kutoa kibali cha kila kudumu ama permanent humanitarian visa , cha milioni moja tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwisho wa mwaka huu. Hatua hii imewezesha sherehe juu ya mchango mkubwa ambao wakimbizi hufanya katika hadithi ya kitaifa ya Australia. Lakini mashirika ya haki za wakimbizi yanasema ni wakati muafaka kufikiria jinsi Australia inaweza kuboresha jibu lake kwa ukimbizi mkubwa wa dunia nzima.
-
Mfumo wa utoaji wa mayai ya uzazi Australia huenda ukabadilika
11/11/2025 Duration: 08minMahitaji ya mayai ya uzazi yanaongezeka nchini Australia kadiri watu wanavyokumbwa na changamoto za uzazi. Lakini mahitaji ya mayai ni makubwa mno kuliko upatikanaji wao na sasa, wataalamu wanapendekeza Australia ifikirie kubadilisha kanuni zinazohusu utoaji mayai.
-
Afya ya akili:kupata usaidizi kama mhamiaji
10/11/2025 Duration: 08minWahamiaji wengi wanakumbana na matatizo tofauti wanapojaribu kupata msaada wa afya ya akili. Umoja wa Mataifa unasema kwamba upatikanaji wa huduma za afya ya akili ni haki ya msingi kwa kila mtu , ikiwemo wahamiaji na wakimbizi. Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba wahamiaji mara nyingi wanakabiliwa na changamoto nyingi kama vile msongo wa mawazo, huzuni, kiwewe na ata upweke kutokana na mazingira mapya. Mtaalamu wa Afya ya Akili Terry Kiguru anatueleza jinsi ya kupata msaada huo na kwanini.
-
Jamii ya Sudan walio Australia waendelea kuwa na wasiwasi
10/11/2025 Duration: 08minJamii ya watu wa Sudan walio nchini Australia wana wasiwasi mkubwa ,wakisubiri habari kutoka kwa familia zao walionaswa katika jiji la Al-Fasher baada ya mlipuko wa ghasia. Jiji hilo lilitekwa na Rapid Support Forces wiki mbili iliyopita, na wataalamu wanaamini kwamba maelfu huenda wameuawa katika mauaji ya kutisha. Kwa kuwa huduma za intaneti na simu zimekatwa, wanaoishi nje ya nchi wanalazimika kukaa na kusubiri ili kujua kama wapendwa wao bado wako hai.
-
Umaskini wa nishati
10/11/2025 Duration: 07minMaelfu ya kaya za Wenyeji kaskazini mwa Australia wanaishi na mfumo wa kulipa kabla wa umeme, ambapo kukatwa kunaweza kutokea wakati wowote. Ripoti mpya sasa imeonya kwamba bila ulinzi wa kutosha, mfumo huu unaweza kuwa hatari katika joto kali.
-
Hali ya hewa inawaathiri pinguini
08/11/2025 Duration: 05minTimu ya kimataifa ya wanasayansi imeonya kuwa pIngwini wanaweza kuwa katika hatari kutokana na madhara ya hali mbaya ya hewa. Utafiti mpya unapendekeza kwamba si tukio moja kama vile joto kali inayosababisha hatari kubwa zaidi, bali ni athari zake zilizoungana pamoja katika ardhi na baharini.
-
Mzio wa karanga kwa watoto upata mwelekeo mpya
04/11/2025 Duration: 07minMiaka kumi baada ya utafiti muhimu kudhibitisha kwamba kuwalisha watoto wachanga bidhaa za karanga inaweza kuendeleza mzio hatari, utafiti mpya umebaini kuwa kuna uwezekano wa kuepuka kuendeleza mizio ya chakula.
-
Serikali kudhibitisha umuhimu wa wahamiaji kwenye uchumi
04/11/2025 Duration: 05minWaziri wa Mambo ya Ndani, Tony Burke, anasema kwamba serikali inafanya kazi juu ya uwezekano wa kutambua ujuzi wa nje ya nchi. Anasema hii itasaidia kuokoa muda na pesa kwa wahamiaji wenye ujuzi wanaotafuta kuhamia Australia. Katika hotuba yake kwa Klabu ya Waandishi wa Habari huko Canberra, Bw. Burke pia ametangaza mabadiliko kwenye akaunti za benki zisizotumika ili kukabiliana na utakatishaji wa fedha.
-
Understanding treaty in Australia: What First Nations people want you to know - Mkataba wa amani: Una maana gani na Una manufaa gani
04/11/2025 Duration: 05minAustralia is home to the world’s oldest living cultures, yet remains one of the few countries without a national treaty recognising its First Peoples. This means there has never been a broad agreement about sharing the land, resources, or decision-making power - a gap many see as unfinished business. Find out what treaty really means — how it differs from land rights and native title, and why it matters. - Waingereza walipowasili Australia walitangaza ardhi kuwa ‘terra nullius’ kumaanisha ardhi isiyomilikiwa na yeyote. Hawakuona haja ya kuzungumza na mataifa ya waaboriginals na kwa hivyo wenyeji wa Australia wanasema kwamba hii ni biashara ambayo haijakamilika.
-
Taarifa ya Habari 26 Septemba 2025
26/09/2025 Duration: 14minWaziri wa Mambo ya Nje Penny Wong amesema Australia ina simama kidete juu ya tamaduni nyingi, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kukosoa uhamiaji katika hotuba yake kwa kikao cha mkutano wa Umoja wa Mataifa.
-
Taarifa ya Habari 23 Septemba 2025
23/09/2025 Duration: 17minWaziri Mkuu amesema ombi la utaifa wa Palestina ni fursa ya amani, katika hotuba yake kuhusu soluhu ya nchi mbili, alipo hudhuria kikao cha Umoja wa Mataifa hii leo Jumanne 23 Septemba 2025.
-
Serikali ya shirikisho yazungumza kwa ukali baada ya kupotea kwa huduma ya simu ya dharura ya Optus
23/09/2025 Duration: 09minWaziri wa Shirikisho wa Mawasiliano amesema Optus inastahili tarajia adhabu kubwa, kufuatia kupotea kwa huduma ya namba ya dharura ya 000, hali ambayo ime husishwa na vifo kadhaa.