Synopsis
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
Episodes
-
Safari ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar
18/01/2025 Duration: 09minZanzibar ilipata uhuru kamili mnamo Desemba 10, 1963, kutoka kwa Uingereza, Waarabu walio wachache walifanikiwa kushika madaraka waliyorithi kutoka kwa Zanzibar kuwepo kama eneo la ng'ambo la Oman.
-
Tanzania: Kuongezeka kwa visa vya ugonjwa wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa
16/11/2024 Duration: 09minWiki hii tunatuwa nchini Tanzania tukiangaza kuongezeka kwa visa vya ugonjwa wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa (UVIDA)
-
Uwekezaji katika sekta ya kilimo mkoani Arusha Kaskazini mwa Tanzania
08/11/2024 Duration: 09minSekta ya Kilimo inaongoza kuwa na fursa nyingi za uwekezaji kwa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla kwa mfano uzalishaji wa Ngano, mafuta ya kupikia, matunda na mboga mboga, mbolea, Viatilifu, mbegu bora, vifungashio, kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno na eneo la kilimo cha umwagiliaji.
-
Tanzania: Kumbukizi ya miaka 119 tangu kuibuka kwa vita vya majimaji
24/10/2024 Duration: 09minKaribu katika Makala ya Afrika mashariki, hii leo tunatuwama nchini Tanzania katika Mkoa Lindi uliopo kusini mwa Tanzania mahali ilipo ibuka vita vya majimaji mara hii ikiwa ni kumbukizi ya miaka 119 tangu kuibuka kwa vita vya Majimaji. Vita vya Majimaji vilipata mizizi yake katika eneo la Nandete Kipatimu, ambapo jamii za Matumbi zilijitokeza kwa ujasiri dhidi ya ukandamizaji wa kikoloni.Roho hii ya upinzani ilichochea moto ulioenea hadi katika eneo la Ruvuma, ambapo watu wa huko, wakichochewa na ujasiri wa majirani zao, walianza kuungana katika mapambano yao wenyewe.Wao pia waliharibu barabara walizolazimishwa kujenga, wakigeuza mandhari ya ukandamizaji kuwa uwanja wa vita kwa ajili ya uhuru.Uasi huu wa pamoja ulionyesha azma inayokua miongoni mwa jamii za kupambana na ukweli mgumu wa utawala wa Kijerumani na kudai heshima yao.
-
Wiki ya vijana ilivyoaadhimishwa mjini Mwanza nchini Tanzania
17/10/2024 Duration: 09minTunaangazia jinsi vijana wanavyoweza kutumia fursa za kidijitali katika kukuza na kuimarisha shughuli zao za kiuchumi mjini Mwanza nchini Tanzania.
-
Tanzania: Mradi wa Jenga Kesho Bora ulivyoanza kutoa mazao kwa wafugaji wa samaki
04/10/2024 Duration: 09minNamna Mradi wa Jenga Kesho Bora (BBT), unaosimamiwa na Wizara ya Kilimo nchini Tanzania ulivyoanza kutoa mazao kwa wafugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria.
-
Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya lugha ya alama
27/09/2024 Duration: 09minJamii imetakiwa kujifunza lugha ya alama ilikuweza kuwasiliana vyema na watu wanaoishi na ulemavu wa kusikia.
-
EAC: Namna mafunzo ya ujasiriamali yanaweza kuwainua vijana
18/09/2024 Duration: 09minKatika Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwama kuangaza na kumulika namna mafunzo ya ujasiriamali yanaweza kuwainua vijana walio ukanda wa Afrika mashariki kupunguza ukali wa Maisha kutokana na kukosa ajira.
-
Maonesho ya awamu ya19 ya biashara katika nchi za Afrika Mashariki
11/09/2024 Duration: 09minMaonyesho haya pamoja na kutoa fursa kwa makampuni ya Afrika mashariki kujifunza na kupanua wigo wa biashara za nje kwakutumia fursa zilizopo za makubaliano ya kibiashara kati ya nchi washiriki nahata kuvuka mipaka ya kufikia juuiya nyingine kwama vile SADC, AGOA,na EBA
-
-
Maendeleo ya shughuli za uvuvi kwenye maziwa Tanganyika na Victoria
28/08/2024 Duration: 09minHivi karibu serikali ya Tanzania iliitaka taasisi ya uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) kuandaa mkakati wa kulifunga ziwa hilo kwa kipindi kirefu. Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya kufunguliwa kwa Ziwa Tanganyika lililofungwa kwa miezi mitatu kutoka Mei 15 hadi Agosti 15, 2024 kwa ajili ya kuruhusu samaki kuweza kuzaliana kwa wingi
-
Hofu kwa wavuvi wa biashara ya samaki Ziwa Victoria nchini Tanzania
28/08/2024 Duration: 09minSerikali ya Tanzania imekuwa ikiteleza kanuni za mwaka 2009 juu ya kulifunga ziwa hilo kwa muda wa siku 10 utaratibu huu umekuwa endelevu hadi sasa ambapo kila mwezi wavuvi hawaruhusiwi kujishughulisha na shughuli za uvuvi kwa siku 10, ikiwa na maana kwamba katika kipindi cha mwaka mzima, Ziwa hilo linafungwa kwa siku 120, sawa na Robo mwaka yaani miezi minne
-
Shughuli za uvuvi zarejelewa katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma
23/08/2024 Duration: 09minShughuli za Uvuvi katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma zilifungwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Mei 15 hadi Agosti 15, mwaka huu lengo likiwa ni kupumzisha ziwa hilo, ili kuchagiza ongezeko la SamakiKufungwa kwa ziwa hilo ni makubaliano yaliyoazimiwa katika kikao kilichofanyika mwaka 2022 kikihusisha nchi zinazozunguka ziwa hilo ambazo ni Zambia, Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
-
Namna siku ya vijana ilivyoadhimishwa katika nchi za Afrika Mashariki
14/08/2024 Duration: 09minSiku ya Vijana Ulimwenguni, ambayo huadhimishwa tarehe 12 Agosti kila mwaka, ilianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka wa 1999 kupitia maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Lengo kuu la siku hii ni kutambua mchango wa vijana katika jamii, kuhamasisha ushirikiano na kuunga mkono haki za vijana, na kuonyesha jinsi vijana wanavyoweza kuchangia maendeleo endelevu na amani duniani
-
Uchaguzi wa urais uliofanyika nchini Rwanda ambapo rais Kagame alitangazwa mshindi
20/07/2024 Duration: 09minKaribu katika Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwama nchini Rwanda tukianga zoezi la kupiga kura lilifanyika Julai 14 na 15, 2024.
-
Harakati za kuelekea uchaguzi mkuu wa urais nchini Rwanda
03/07/2024 Duration: 09minRaia wa Rwanda ambao ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki, kwa sasa wapo katika kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu Uchaguzi utakaofanyika Julai 15, 2024 kumchagua rais wao mpya Pamoja na wabungeRais anayemaliza muda wake Paul Kagame anawania kwa muhula wa nne akisaka ridhaa ya Wanyarwamda kusalia katika Ikulu ya KigaliTaifa la Rwanda linalo kadilikuwa na jumla ya wakazi 14,410,469 kati yao ni Wanyarwanda takribani milioni 9 wameandikishwa katika daftari la mpiga kura kushiriki katika uchaguzi Urais, Jambo lenye sura mpya kwa sasa ni kwa mara ya kwanza uchaguzi huo utafanyika sambamba na ule wa bunge.
-
Changamoto za raia wa Afrika Mashariki kupata maji kwa ukaribu
28/06/2024 Duration: 09minMakala ya Afrika mashariki ikiangazia juu ya namna wakazi wa Jumuiya ya Afrika mashariki wakiwa katika mkwamo wakupata katika huduma ya maji kwa ukaribu licha uwepo wa vyanzo vikumbwa vya maji. Kwa mujibu wa tovuti ya Jumuiya ya Afrika mashariki, Maziwa makubwa yote mawili kwa maana ya ziwa Victoria na Tanganyika, na hatimaye, Mto White Nile hutegemea vyanzo vya maji vya kikanda vinavyojulikana kama Minara ya maji Water Towers ya eneo hilo.Minara ya Maji ya Afrika mashariki ni mkusanyiko wa mazingira ya milimani na mabonde ya mito yanayohusiana.Maeneo haya yana ushawishi mkubwa kwa hidrolojia ya kikanda na mizunguko ya hali ya hewa duniani.Licha ya uwepo wa minara hii bado serikali za wanachama wa jumuiya hii zipo katika mkwamo wakufikisha huduma za maji kwa wananchi walio wengi.
-
Tanzania: Kufungwa kwa muda kwa uvuvi ndani ya Ziwa Victoria
22/06/2024 Duration: 09minSerikali inasema hatua hiyo ya kufungwa kwa giza inalenga kuwapa nafasi samaki wadogo kua.
-
Mvutano kati ya Somalia na Ethiopia kuhusiana na suala la Somaliland
08/06/2024 Duration: 09minKatika Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwa pembe ya Afrika tukiangaza juu ya vuta nikuvute katika serikali ya mjini Mogadishu na Addis Ababa.
-
Kumbukizi ya miaka 28 tangu kuzama kwa meli ya MV Bukoba
01/06/2024 Duration: 09minBaadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kushiriki ibaada ya kumbukizi ya ajali ya MV Bukoba, ibada hiyo imefanyika katika Makaburi ya wahanga wa ajali ya MV Bukoba yaliyopo katika kitongoji cha Igoma Mkoani Mwanza nchini Tanzania