Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

ACS2: Addis Ababa: Vijana wasisitiza uwekezaji kwenye ajira za kijani

Informações:

Synopsis

Uchumi wa kijani ni miongoni mwa mada kuu zilizojadiliwa kwenye mkutano wa pili wa mazingira wa bara la Afrika uliofanyika hivi majuzi jijini Addis ababa, ambapo wajumbe walijadili mikakati ya kufadhili maendeleo ya kijani barani Afrika kupitia masuluhisho yanayotegemea asili, teknolojia safi. Mjadala umeibuka kuhusu nafasi ya vijana katika mipango ya serikali za Afrika kuelekea uchumi wa kijani, kupitia ajira za kijani.