Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Mkataba wa plastiki: Mgawanyiko kuhusu jinsi ya kukabiliana na hatari ya kiafya na kiikolojia.
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:09:56
- More information
Informações:
Synopsis
Mataifa mbalimbali ulimwenguni yameombwa kuchukua hatua na kutatua mzozo wa kimataifa wa plastiki, mwenyekiti wa kamati ya majadiliano ya kiserikali, mwanadiplomasia wa Ecuador, Luis Vayas Valdivieso akiwaomba wadau waliokusanyika Geneva, Uswizi kwa siku 10 kuunda mkataba wa kihistoria wa kuzuia uchafuzi wa plastiki. "Uchafuzi wa plastiki unaharibu mazingira, unachafua bahari na mito yetu, unatishia viumbe hai, na unadhuru afya ya binadamu," alisema Valdivieso. Wataalam pia katika ripoti iliyochapishwa kwenye Jarida la matibabu la Lancet, wameonya kuwa uchafuzi wa plastiki ni "hatari kubwa, inayokua na isiyotambulika" kwa afya ambayo inagharimu dunia angalau dola trilioni 1.5 kwa mwaka. Bonyeza hapo juu kusikiliza wito wa watetezi wa mazingira kuhusu umuhimu wa kupatikana kwa mkataba wa plastiki.