Gurudumu La Uchumi

Kodi ya lipa Kadiri unavyopata (PAYE): Athari kwa wafanyakazi na waajiri

Informações:

Synopsis

Msikilizaji wakati dunia ilipoazimisha siku ya kimataifa ya wafanyakazi, viongozi barani Afrika na hasa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki walitangaza nyongeza ya mshahara huku wengine wakitoa ahueni ya ushuru wa mapato. Kwenye makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunaangazia kodi ya lipa kadiri unavyopata (PAYE) kwa wafanyakazi na waajiri. Kuzungumzia hili msikilizaji kwenye line ya simu nimemualika Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.