Siha Njema

Kukata kiu ya jamii zinazoishi mpaka wa Kenya na Somalia ,waathiriwa wa mgogoro

Informações:

Synopsis

Mamia ya wakaazi wa kaskazini  mashariki mwa Kenya maeneo yanayopakana na Somalia na waathiriwa wakubwa wa mzozo wa Somalia hawajakuwa na maji masafi , hali hiyo ikizidisha mgogoro wa kijamii ndani ya jamii hii ya wafugaji wanaotokea upande wa Kenya na  upande mwingine wa Somalia. Kukabili hali  hii ,kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu , International Committee  of the Red cross ,ICRC , shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya ,Kenya Red Cross,KRC katika mkakati wa kuleta amani na ustawi imekuwa ikifanya miradi ya kuwapa wakazi maji .Carol Korir amezuru eneo la Masalani ,kaunti ya Garissa  kilomita chache na msitu wa Boni  ambapo Al shabab wamekuwa wakifanya mashambulizi  na kujificha .