Jua Haki Zako

Kenya : Haki za watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi wanataka kutambuliwa zaidi

Informações:

Synopsis

Katika makala  haya ni awamu ya pili tunaendelea na mazungumzo yetu na bwana meshaka Sisende raia wa Kenya anayeishi na ulemavu wa ngozi. Juma lililopita tuliangazia pakubwa changamoro wanazopitia raia hawa naoishi na ulemavu wa ngozi na hapa tunazidi kuangazia mananikio ya raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi.Miaka kadhaa iliopita  mauwaji ya raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi yalikithiri sana nchini Tanzania, hatua iliochangia viongozi wa tabaka mbalimbali kusimama kidete kukemea mauwaji hayo mamlaka nazo zikiwakamata waliokuwa wakihusishwa na mauaji hayo kwa misingi ya kishirikiana. Ni hapo ndipo wasanii kama vile Herbert Naktare maarufu Nonini kutoka nchini Kenya aliachilia wimbo wake wa Colour Kwa Face, kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwakumbatia watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.