Gurudumu La Uchumi

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 3:58:42
  • More information

Informações:

Synopsis

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .

Episodes

  • Sehemu ya II: Umuhimu wa kuwa na nidhamu ya kuweka akiba ya fedha

    08/01/2025 Duration: 10min

    Hivi leo ni sehemu ya pili ya makala ya Gurudumu la Uchumi, hasa tunapouanza mwaka 2025 tunaenda kujadili kuhusu nidhamu ya kuweka akiba ya fedha, ufanye nini kuongeza kipato, unatumiaje fedha ulizonazo kuwekeza ? Haya ni baadhi ya mambo ambayo tutaenda kuyatazama kwenye makala ya juma hili. Tutakuwa na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.

  • Sehemu ya I: Kwanini ni muhimu kuwa na nidhamu ya kuweka akiba ya fedha

    01/01/2025 Duration: 09min

    Heri ya mwaka mpya 2025 msikilizaji wa RFI Kiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu na hasa makala ya Gurudumu la Uchumi, ni imani yetu kuwa nyote mbuheri wa afya. Makala ya Gurudumu la Uchumi, tutajadili kuhusu nidhamu ya kuweka akiba ya fedha. Kuzungumzia hili msikilizaji kwenye line ya simu nimemualika Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.

  • Nidhamu ya matumizi ya fedha

    25/12/2024 Duration: 10min

    Katika makala ya hivi leo, tunajadili kuhusu umuhimu wa kuwa na nidhamu ya fedha, kwanini ipo haja ya kuwa na nidhamu ya matumizi binafsi, vipi unaweza kujipanga kwa mwaka ujao? Haya ni miongoni mwa maswali ambayo mtaalamu wetu wa uchumi na biashara Ali Mkimo anaenda kuyajibu.

  • Akina mama jimbo la Migori nchini Kenya wanzisha kiwanda cha kuchakata samaki

    19/12/2024 Duration: 09min

     Makala haya yanazungumzia hatua za  wanawake na wasichana katika eneo la Opapo, Kaunti ya Migori nchini Kenya, kwa msaada wa mashirika yasiyo ya kiserikali  na serikali ya kaunti, wameanzisha kiwanda  cha kuchakata samaki, kuboresha biashara ya samaki, na kuongeza thamani kwa kutengeneza bidhaa kama soseji na baga,hivyo kuinua uchumi

page 2 from 2