Jukwaa La Michezo

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 9:31:07
  • More information

Informações:

Synopsis

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali. 

Episodes

  • Mashindano ya kukimbiza magari, yapamba moto nchini Kenya

    22/03/2025 Duration: 23min

    Mashindano ya dunia ya kukimbiza magari, Safari Rally yanaendelea nchini Kenya. Madereva mbalimbali  kutoka  duniani, wanakutana mjini Naivasha kwa ajili ya kutafuta ubingwa wa mwaka 2025.

  • CAF: Motsepe achanguliwa tena kuwa rais kwa muhula wa pili wa miaka minne

    15/03/2025 Duration: 23min

    Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na uchaguzi wa CAF, uwanja wa Mkapa wafungiwa kwa muda, michuano ya kufuzu dimba la dunia kwa kina dada chini ya umri wa miaka 17, maandalizi ya mashindano ya kuendesha magari ya WRC Safari Rally, uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya hatua ya kumi na sita bora naye Neymar alazimika kuaga kikosi cha Brazil kufuatia jeraha

  • Misri, Morocco,Tunisia zang'ara mashindano ya tenisi ya vijana chini ya miaka 14

    02/03/2025 Duration: 23min

    Tuliyokuandalia hii leo ni pâmoja na matokeo ya mashindano ya tenisi ya vijana barani Afrika chini ya miaka 14, kocha mpya wa Kenya ni nani, matokeo ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada, timu sita kushiriki ligi ya Afrika ya basketboli kwa mara ya kwanza, huku Afrika Kusini ikijiandaa kutuma ombi rasmi la kuandaa mkondo mmoja wa F1 na Jose Mourinho apata afueni baada ya adhabu yake kupunguzwa.

  • Simba kukutana na Al Masry kwenye Droo ya robo fainali Kombe la Shirikisho CAF

    22/02/2025 Duration: 23min

    Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na matokeo kwenye mashindano ya kimataifa ya gofu ya Magical Kenya Open, bondia wa DRC kupambana na muingereza huko Saudi Arabia, maandalizi ya Tour du Rwanda, Droo ya robo fainali michuano ya klabu bingwa Afrika, mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada 2026 na basketboli ya 2025, halikadhalika Droo ya 16 bora mechi za klabu bingwa Ulaya na michuano ya raga ya Vancouver 7s.

page 2 from 2