Synopsis
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
Episodes
-
Kenya : Haki za watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi wanataka kutambuliwa zaidi
17/06/2024 Duration: 09minKatika makala haya ni awamu ya pili tunaendelea na mazungumzo yetu na bwana meshaka Sisende raia wa Kenya anayeishi na ulemavu wa ngozi. Juma lililopita tuliangazia pakubwa changamoro wanazopitia raia hawa naoishi na ulemavu wa ngozi na hapa tunazidi kuangazia mananikio ya raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi.Miaka kadhaa iliopita mauwaji ya raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi yalikithiri sana nchini Tanzania, hatua iliochangia viongozi wa tabaka mbalimbali kusimama kidete kukemea mauwaji hayo mamlaka nazo zikiwakamata waliokuwa wakihusishwa na mauaji hayo kwa misingi ya kishirikiana. Ni hapo ndipo wasanii kama vile Herbert Naktare maarufu Nonini kutoka nchini Kenya aliachilia wimbo wake wa Colour Kwa Face, kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwakumbatia watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
-
Haki za raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi hapa Africa
12/06/2024 Duration: 09minKila mwaka Juni 14 dunia huadimisha siku ya watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi sherehe zilizoanza kuadimisha tangu mwaka 2014, ili kuhamasisha jamii kwamba watau wanaoishi na ulemavu wa ngozi wao ni watu wa kawaida katika jamii. Katika makala haya Meshaka Sisende kutoka nchini Kenya anasimulia maisha ya kawaida ya watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya
-
Tume ya haki za binadamu nchini Uganda yatuhumiwa kuegemea upande wa serikali
31/05/2024 Duration: 09minMakala haya yanaangazia tendekazi wa tume za kutetea haki za biandamu za serikali zetu za Africa mashariki.Hii ni baada ya lalama kutoka kwa kiongozi wa upinznai nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine kwamba tume ya haki nchini Uganda imekuwa ikiegemea upande wa serikali katika kutekeleza majukumu yake. Robert Kyagulanyi,amelazimika kuondoa lalama zake mbele ya tume ya haki ya kutetea haki za biandamu nchini Uganda kutokana na madai inayosema tume hiyo imeshindwa kuyashughulikia.Wine alikuwa amewasilisha kesi yake mwaka 2018 akilalamikia hatua ya polisi nchini Uganda kukiuka haki zake kwa kumzuia kuandaa tamasha za muziki zaidi ya 20, mbali na polisi kuchukuwa nyombo vyake vya mziki, hili akidai lilimzuia kupata haki yake ya kupata mapato kutokana na mrengo wake wa kisiasa. Fahamu mengi kwa kuskiza makala haya.
-
Kenya : Unyanyapaa wanaopitia kina mama tasa kwa jamii
21/05/2024 Duration: 10minKatika makala haya tunaangazia haki za kina dada ambao hawajafanikiwa kupata watoto katika jamii zetu za kiafrica. Barani Afrika wanawake ambao hawana uwezo kupata watoto au wale huchukuwa muda mrefu kupata watoto , hupitia changamoto si haba ,na kukosa haki,kama vile kutotambuliwa na jamii,uridhi wa Mali na hata wengine kufukuzwa kwenye ndoa,hali hiyo ikichochewa na tamaduni ambazo zimekita mizizi. Kwa mjibu wa twakwimu za shirika la afya duniani WHO ni kwamba wanawake 15 kati ya 100 barani Afrika hawana uwezo wa kupata watoto, na kati ya wanawake 6 angalau mmoja huwa hawana uwezo wa kupata mtoto kidunia.Swala la kukosa kupata mtoto hushuhudiwa kati ya wanawake na wanaume, ila hapa barani africa kasumbuka mara nyingi huelekezewa kina mama, hili likisababisa dhiki, unynyapaa, ufukara miongoni mwa wanawake wengi wao sasa wakiathiriwa na afya ya akili na hata kisaikolojia.Licha ya tatizo hili kuwa na suluhu, wengi wamesalia kukosa imani kutokana kwani hawana pesa za kutafuta tatibu husika.Kufahamu mengi zaidi