Synopsis
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
Episodes
-
COP29: Wanamazingira wapendekeza ufadhili zaidi kwa Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
19/11/2024 Duration: 09minMkutano wa hali ya hewa COP29 ukiendelea nchini Azerbaijan, masuala yanayoibua changamoto ni ufadhili, mchakato wa kuondokana na mafuta kisukuku, athari ambazo zimekumba bara la Afrika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, kuongezeka kwa viwango vya joto lakini pia suluhu zinazopendekezwa na wataalam wa mazingira. Kauli mbiu ya mwaka huu kwenye mkutano wa COP29 ni uwajibikaji wa ufadhili haswa kutoka mataifa tajiri ambao wanachangia kwa viwango vikubwa uchafuzi wa mazingira wakati athari zake zinaathiri nchi zisizojiweza na shirika la mazingira la Greenpeace Africa linapendekeza mustakabali wa nishati mbadala na haki ya hali ya hewa kwa Afrika.Kwa mengi zaidi bonyeza ili kusikiliza makala.
-
Ripoti ya mazingira ya UNEP kuhusu pengo la uzalishaji wa gesi chafu duniani 2024
31/10/2024 Duration: 10min -
Jamii Pwani ya Kenya wapinga mradi wa nyuklia kutokana na athari kwa mazingira
29/10/2024 Duration: 09min -
DRC:Jamii ya mbilikimo wakemea uharibifu wa misitu unaofanywa na makundi ya waasi
09/10/2024 Duration: 10min