Synopsis
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Episodes
-
Tundu Lisssu afunguliwa kesi ya uhaini, CHADEMA matatani
16/04/2025 Duration: 09minMwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, Tundu Lissu, Aprili 10 alifunguliwa kesi ya uhaini, baada ya kukamatwa akiwa kwenye kampeni ya kisiasa, kushinikiza mageuzi kwenye mchakato wa uchaguzi, uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba.
-
Tanzania: CHADEMA yashinikiza mabadiliko kabla ya Uchaguzi Mkuu
09/04/2025 Duration: 09minMwezi Oktoba 2025, wananchi wa Tanzania, watashiriki kwenye uchaguzi Mkuu, kuwachagua madiwani, wabunge na rais. Hata hivyo, chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, kinashinikiza mageuzi kwenye sheria za uchaguzi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.Je, kitafanikiwa katika harakati zake ?
-
Mkuu wa majeshi nchini Kenya akemea wanaomtaka rais Ruto aondoke
02/04/2025 Duration: 10minMkuu wa Majeshi nchini Kenya, Jenerali Jenerali Charles Kahariri na Mkuu wa idara ya ujasusi Noordin Haji, wameonya dhidi ya kampeni inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii na mikutano ya hadhara ya –Ruto Must Go- au Ruto lazima aondoke, inatishia hali ya kisiasa nchini Kenya na ni lazima, ikome.Je, jeshi la Kenya linaingilia siasa ? Tunajadili…
-
Harakati za kumaliza mzozo wa DRC, nani atafanikisha ?
26/03/2025 Duration: 10minWiki hii tunaangazia kinachojiri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya Angola kujiondoa kama mpatanishi wa mazugumzo ya mzozo wa Mashariki mwa nchi hiyo, rais Paul Kagame na Tshisekedi wakutana Doha na mazungumzo ya kisiasa yanayolenga kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, yazinduliwa jijini Kinshasa.Wachambuzi wetu ni Mali Ali, akiwa Paris na Francois Alwende akiwa jijini Nairobi.