Synopsis
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episodes
-
Bidhaa mpya za tumbaku zinauzwa kwa mwoneko bora, ladha ya kuvutia kuficha madhara yake
06/08/2024 Duration: 09minKuuza bidhaa za tumbaku za kisasa ,kama bidhaa zisizo na madhara ,kutumia ladhaa tamu na kutumia mitandao ya kijamii kuuza bidhaa hizi ni mbinu ambao kampuni za kutengeneza tumbaku zinatumia kuwavutia vijana na kuwa wateja wao wa kudumu. Kampuni hizi zinafadhili pia utafiti ambao unakinzani na utafiti wa taasisi za afya kuhusu madhara ya Tumbaku.Isitoshe kampuni hizi zinazalisha bidhaa ambazo mtumiaji anaweza kutumia zaidi ya moja .
-
Mbinu fiche zinazotumia sekta ya kuzalisha tumbaku kuendelea kudumu soko
01/08/2024 Duration: 10minKumeshuhudia juhudi makhsusi kutoka sekta ya Tumbaku zinazopinga sheria zinazodhibiti Tumbuka kama vile kupitia ushuri au sheria zenye adhabu kali Sekta hii pia imeonekana kurubuni serikali tofauti kwa kutoa msaada bila wao kufahamu lengo la sekta hiyo. Aidha kuna tafiti za kisayansi zinazofadhiliwa na sekta hii kukabili sayansi zinazorodhesha tumbaku na bidhaa za sigara kuwa zenye madhara makubwa ya kiafya
-
Simulizi kuhusu ugonjwa wa Endometriosis unaowasababishia wanawake maumivu
24/07/2024 Duration: 10minUgonjwa wa Endometriosis hudhihirika msichana anapovunja ungo na huja na maumivu makali kabla ,wakati na hata baada ya hedhi Lilian Leley ameishi na maumivu hayo kwa zaidi ya miaka thelathini.Amefanya upasuaji mara mbili na anatazamiwa kwenda kwenye operesheni nyingine hivi karibuni katika kujaribu kutafuta tiba ya ugonjwa wa EndometriosisAnasimulia masaibu yake ,ambapo anasema ndani ya mwezi huenda ni mzimu tu kwa siku 10
-
Fahamu kuhusu ugonjwa wa Endometriosis na changamoto za afya zinazofungamana nao
16/07/2024 Duration: 10minEndometriosis hutokea wakati tishu kwenye ukuta wa tumbo la uzazi zinapopatikana katika maeneo mengine ya mwili ikiwemo mapafu ,utumbo na hata ubongo Endemotriosis huwa na dalili zinazofanana magonjwa mengine ya uzazi na unaweza kubainika kupitia kipimo cha Laparoscopy ambapo tishu hizo zinachunguzwa moja kwa moja