Synopsis
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Episodes
-
Sanaa ya Uchongaji Vinyago nchini Tanzania
16/11/2024 Duration: 20minSteven Mumbi amezungumza na Lyala Sebastian Mchongaji wa Sanaa za Vinyago.
-
Sanaa ya uchoraji wa vinyago na fursa wa biashara inazoleta
09/11/2024 Duration: 20minWabunifu wa Sanaa ya Uchongaji Vinyago wamewekeza katika kung'amua fursa ya biashara kwa Mataifa ya Afrika Mashariki ili kujikwamua na vipato Duni, Steven Mumbi amezungumza na Mintanga Ramadhani Msanii wa Sanaa za Uchongaji Vinyago kutoka nchini Tanzania.
-
Muziki wa HIP HOP nchini Tanzania
26/10/2024 Duration: 20minMuziki wa HIP HOP nchini Tanzania umefifia kutokana na ugumu wa kufanya Muziki huo,Msanii PMawenge anasimulia hatua za kuchukua kuurejesha sokoni katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
-
Tanzania: Sanaa ya ushairi na msanii Michael James maarufu Michael
28/09/2024 Duration: 20minSanaa ya ushairi inawavutia zaidi watu wanaotamani kujua utamu na upekee wa lugha adhimu ya Kiswahili, Chuo kikuu cha Dar es salaam kimewatambua na kuwapa fursa vijana waliosomea fani ya sanaa, kubobea katika kughani Mashairi. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Msanii Michael James maarufu Michael.